BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

Baba nchi ya wote hii, na hiyo siyo excuse. Elewa kuwa hata tunapowalalamikia wazungu kuwa wanatukandamiza, wao wanaona halali kwa vile maendeleo yote ya teknolojia yameanzishwa kwao, na nyie ni wa kutumiwa tu.

Na mambo kama hayo ndio yalikuwa chanzo cha ugomvi Rwanda na Burundi. Mkiwa mmeichoka amani OK. lAKINI KAMA NI WAPENZI WA AMANI BASI NJIA PEKEE NI MAZUNGUMZO.
 
unaijua BAKWATA wewe.acha ushabiki wa kijinga.Bakwata haiwakilishi waislamu bali ni taasisi ya serikali inayotumika kudhibiti waislam.

light travels faster than sound,that' why some people appears to be bright untill you hear them speak
 

Precisely! Mifano ni mingi sana hapa nchini. Kuna mikoa (na hiko mingi) ambayo kama wwe sio mzawa wa huko kupata ubunge katika majimbo ni kama ngamia kupita katika tundu la sindano. Mikoa kama Kagera, Kilimanjaro, Mbeya nk ni "conservative". Haijarishi kama wewe dini yako ni minority katika sehemu hizo iri mradi uwe ni mzaliwa wa kule.

Na hii ya kusema kwamba wabunge waislam katika Bunge la Tanzania ni wachache ni kweli? Au wabunge toka Zanzibar sio wabunge? Kama ni wabunge tena waisalam kwa nini hawahesabiwi? Hizi tuhuma za upendeleo hazikuanza jana. Kuna wakati mwalimu Nyerere alituhumiwa kuwapendela wakatoliki katika baraza lake la mawaziri. Alipofanya hesabu akakuta katika mawaziri wake zaidi ya ishirini kulikuwa na wakatoliki wawili tu na hata hivyo kati yao mmoja hakuwa mkatoliki safi mana alikuwa ameoa wanawake wawili!

Ukijaribu kufanya tadhimini kidogo utaona kwamba hizi takwimu zinazotajwa hapa ni za mijini zaidi bila kuzingatia hali ya vijijini (hasa bara) ikoje.
 
Huo waraka uko wapi?
Tuwekeeni hapa, kwanza tuusome ndipo tuujadili
 
WanaJF hapa nasisitiza tunajadili kitu gani?Huu sio WARAKA ni DUKUDUKU LANGU au SEMA USIKIKE.Kama unamjua opponent wako huna haja ya kubishana nae,ile kumfahamu tu inatosha!Kila kitu kipo wazi,tunafahamu ni kwa nini wazungu wametuzidi,so kuna lawama hapo,alaumiww nani??au ni kujitahidi kusonga mbele au kulala basi! inasikitisha watu wenye bongo zao kutoa maneno kama hayo,well I'm sure hamgusi yeyote mwenye akili wala haimwingii kichwani so its in vain kama waislamu mtaendelea namna hii,iga mfano wa waislam wa Dubai,Saudia,Kuwait etc!Boko haramu hawatakiwi hapa!
 

Hivi unaonaje ukatupa at least title tu ya hicho chanzo cha takwimu ili tuende tukakitafute sisi wenyewe? au waonaje bibie? vigumu au?

NB: Kushindwa kwako kuitetea hii hoja kutakufanya uingie kwenye list yangu ya watu wasio na input.
 

Hivi kiswahili ni lugha yako ya ngapi?

Nimesema hawa watu wapuuzwe na hoja zao muflis . Sikusema wapuuzwe alltogether na ndio maana nikasema hawa waangaliwe kwa macho matatu maana ndio Boko Haram wa kesho hawa. A

Kalaghabaho.
 
Basi kumbe kigeuke kibao 2010 wabunge waislam 96%, wakristo wawe 4%. Ila sijui mgawanyo uwe vipi kwa waislamu, tufanye Shia 75%, Suni 20% madhehebu mengine 1% na wakristo waambulie 4% kama kawa. Je, imekaa sawa?

Huko ndiko kufilisika akili. waislamu tuendelee kutilia mkazo madrasa wakati wakristo wanakazia kupeleka shule watoto wao, halafu sie tutetee sana dini katika kila kitu, kama vile tumeandikiwa kwamba mtu ataenda mbinguni kwa kupitia ubunge pia.

Sikusikia wakatoloki wakija na hoja za kidini katika waraka wao. Sijui kwa nini mashura hao hawakuwatumia wataalam wasomi waislam ili kufikiri zaidi kabla ya kuandika? Au masheh ndio walioandika misikitini?

Leka
 
Kama utakuwa makini utagundua kuwa mwangwi wa nyaraka hizi za kidini haujaja kwa bahati mbaya, kuna upungufu mkubwa katika utendaji wa serikali yetu kiasi kwamba watu wanatafuta njia ya kuziba mwanya ili maisha yaende. Kimsingi cha kufanya sio kumlaumu pengo au ashura ya maimamu, ni wakati wa kutafakari upungufu uko wapi na kujaribu kuziba upungufu huo ili mambo yaende. Wanasiasa wanajidanganya sasa tena mno wanafikiri wao ndio wenye watu, bilakujua dini ndizo zenye watu na watu ni watii zaidi kwa dini kuliko siasa kwani ndizo zinawapa comfort na relaxation wakati wa shida zao na si serikali ambayo hasa ndiyo ilitakiwa kunusuru watu hoa, lakini kwa bahati mbaya imejaa watu wenye kejeri, ujuaji, kibri, wezi na wabnafsi. jambo hili limewakera watu wa dini ambao ndiyo wahanga namba moja katika kuzituliza roho hizi zilizochoshwa, na kama walezi lazima watafute namna ya kunusuru watu. Binafsi watu wa dini wamefanya kazi yao kwa haki kubwa kunyesha udhaifu wa serikali na asiwepo mtu wakuwalaumu hawa na walaumimiwe watawala na siasa zao.
 

kama Jf ingekuwa na tuzo ya mchango wenye mantiki kwa wiki basi mimi ningekupendekeza wewe uipate kwani , watu wengi wanatazama haya mambo yanayojili tz kwa juu juu tu! na watu wengi wanakuwa kama wanalopoka ili kufanya yaishe au bora liende, wengi wetu hatuangalii haya matatizo kiundani na kujadili tutatuweje na tufanyenje kwa manufaa ya jamii na baadae.
nilikuwa naamini Jf ni baraza la wasomi na wasomi wanaangalia vitu kiundani huku wakibishana kwa mantiki lakini naona Jf bado ni baraza la siasa..
 
Unajua kuna watu imani zimewapofusha macho kiasi kwamba hata mtu wa imani yake akizungumza ujinga wa namna gani yeye atamtetea tu na anaweza kwenda mbali hata kuwaponda wale wanaotoa hoja za maana. Kwa mfano Lipumba aliuponda sana waraka wa Wakatoliki bila hata kuuchambua lakini huyo huyo anasema waraka wa Waislamu umezungumzia baadhi ya mambo ya muhimu kama marekebisho ya katiba na tume huru ya uchaguzi!! Kwa nafasi yake alipaswa kuchambua anachokipinga yeye ni contents za hizo nyaraka au source? Anataka kusema waraka wa Wakatoliki hauna "chochote" cha maana? Huku ni kujichanganya sana, na kwa Lipumba sishangai! Ni mwepesi sana wa kuhusisha maslahi yake binafsi (kiimani,kisiasa, kifedha) na yale ya kitaifa, badala ya kuyatenganisha.

Vivyo hivyo akina Makamba na Kingunge, walipaswa kushikiria misimamo yao kuwa nyaraka za kidini hazitakiwi kuliko kusema eti no comment kwa waraka mmoja halafu waraka mwingine unakuwa mwepesi kuuzungumzia bungeni. Naomba kuwapongeza Bakwata kuonesha msimamo wenye afya kwamba kama walipinga waraka wa dini wataendelea kupinga nyaraka zote za namna hiyo. Huo ndio msimamo! Tunatakiwa kuwa "holistic" na kuepuka double standard.
 

Hapo kaka umesema. Na katika elimu hali ni hiyohiyo. Kuna waislamu wapare, wachaga, wahaya, wahehe: hawa wamesoma kama wenzao wengine wa maeneo hayo na wanazo nafasi nzuri mbali mbali. Kuna wakristo wamakonde, wafipa, wasafwa, wasandawi: kama wenzao wa maeneo hayo, hawa wanasota tu na elimu kiduchu au ngumbaro.

Kumbe badala ya kulalamika dini, dini, nk, tufanye bidii za kuendeleza maeneo yetu, au tupiganie maendeleo yenye uwiano unaokubalika wa kijiografia. Hilo likifanikiwa kila mtu atafaidika na si dini wala upuuzi huu mwingine.
 
Enyi NDIVYO TULIVYO, silikilizeni kwa makini.
waraka zote hizi ni changa la macho na litazidi kutugawa zaidi ya kutuunganisha. Hadi sasa hivi waraka zote mbili ni Ushindi kwa CCM kwani habari zinazozidi kusambaa mjini ni kwamba waraka wa kanisa ulikuwa shinikizo la Chadema na ndio maana hawakuupinga, Hivyo CUF nao wakaunda shinikizo lao kwa kutumia Waislaam kuunda waraka wao.

Wakuu hizi ni tuhuma mbaya sana zenye kiwango kikubwa cha utenganisho wala sijapata kusikia. Iwe kweli au Uongo tatizo ni vyombo vya dini kuingilia siasa mahala sii pake..Na ndio kinachojenga Udini, mada hii na ile ya waraka wa kanisa zote zimejaa fikra za Udini, watu kwa makundi na ushabiki wa dini kujenga hoja za watu...Yote haya yametokana na hizi waraka..Matusi, majigambo, unafiki na machafu yote yanayozungumzwa humu JF ni dhambi kubwa kwa wahusika wa waraka hizi kwani kama sii wao JF kusingekuwepo na Mgawanyiko huu.

Hapa Udini umeshaingia na ndicho nilichokuwa nikisema toka awali kwamba mtu yeyote ambaye haoni Ubaya ya waraka hizi ni mtumwa wa mawazo, ni ktk fungu la Ndivyo Tulivyo.
Nimekuwa nikisisitiza siku zote kwamba unapotaka kufanya kitu chochote ni muhimu sana kuzingatia WATU na MAZINGIRA yake, hizi waraka zote ni matokeo ya watu ambao walipuuza kutazama watu na mazingira na matokeo yake zitaibomoa jamii yetu badala ya kuijenga.

Kwani hata Vita ya Rwanda ilianzishwa na waraka..viongozi wa dini wakidai wao wamepewa wahi na Mungu kuchagua viongozi, kupigania haki zao na kadhalika matokeo yake wamekufa mamillioni ya watu kwa propaganda mbaya na chafu wakitumia dini.

Wakuu zangu kuweni waangalifu sana, Sasa hivi mshindi na anayeonekana wa maana ni CCM, ambaye hakubali waraka wa Kanisa wala wa Waislaam. Kwa maana hiyo inaonyesha wazi Chadema ni wadini na CUF ni wadini, hii ndio picha wanayoipata wananchi wasiopenda vita ya Udini..
 
Last edited:
Mkandara,

..wapi CCM wamepinga waraka wa kina Shekhe Ponda?

..Mzee Ngombale Mwiru alifikia mpaka kuchana-chana waraka wa Wakatoliki ndani ya vikao rasmi vya CCM, mbele ya Mwenyekiti,Makamu,Katibu Mkuu etc etc.

..kwamba Ngombale Mwiru hajauchana waraka wa kina Shekhe Ponda maana yake anauunga mkono au nini?

..Makwaia Kuhenga yuko wapi naye na makala zake za kushutumu Wakristo kwa kuwa intolerant kwa imani nyingine? huyu aliandika makala ktk Daily News gazeti la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

..hivi aliyempa nafasi Makwaia kuandika makala ile alikuwa anaelewa kwamba Daily News ni gazeti la serikali?

NB:

..kwa mtizamo wangu mpasuko wa Kidini ulianza miaka ya 80, ambako kuliibuka vikundi vya kidini vilivyojikita ktk kutoa kasoro vitabu vya mafundisho vya dini nyingine.

..unakuta mtu anaamini dini "X," sasa badala ya kuhubiri kutoka ktk vitabu vitakatifu vya dini yake, anatumia muda mwingi kutoa kasoro na kubeza maandiko ya dini "Y."
 
Hii equation imekaeje? Ponda dhidi ya CCM;
Ponda dhidi ya Wakatoliki;
Wakatoliki dhidi ya CCM;
BAKWATA dhidi ya Ponda;
Kinguge (CCM) dhidi ya Wakatoliki;
Majibu ni nini katika mustakabali wa kisiasa nchini?
 
Jokakuu,
Mkuu wangu jaribu kusoma na kuelewa nini nimeandika..
Mimi nawakilisha habari za mitaani jinsi vitu hivi vinavyopamba moto kuwa waraka wa kanisa ni habari ya Chadema na waraka wa Waislaam ni mpango wa CUF. Iwe kuna ukweli au hakuna hilo mimi sielewi hadi hapo pengine kanisa la Warutheli nalo liaandike na isemekane wameshinikizwa na CCM.. lakini hadi sasa hivi kinachojulikana ni kwamba waraka wa kanisa ni madudu ya Chadema na waraka wa waislaam ni CUF.. CCM haipo uwanjani hivyo washabikie, wasishabikie haina maana wanaupokea waraka wa waislaam isipokuwa wanajua jinsi ya kucheza rafu Politics. CCM wanamjua adui yao wakati wapinzani hawafahamu wanachojichimbia wenyewe!

Mkuu wangu nitakuwa mfano mzuri na mdogo tunaofanya kila siku..Washabiki wa Arsenal siku zote watakuwa against Manchester hata kama ManU itacheza na team ya Urusi. Hii haina maana washabiki wa Arsenal ni wapenzi na wanawapokea team ya Urusi kuwa ni wenzi wao ama wanakubaliana na uchezaji wao isipokuwa anything against Manchester is worth betting for!
Now, CCM wanajua fika kwamba chochote kile against Chadema ni ushindi kwao na kutokea kwa waraka huu wa Waislaam ndiko kumewapa nguvu zaidi kwani kinachoonekana hapa ni Chadema na CUF.. CCM ni watazamaji tu yaani washabiki.

Halafu maswala ya Udini ya mwaka 80 sidhani kama yanahusiana lolote na hapa..Dini ni ELIMU na nakuhakikishia kwamba nayajua mengi ktk Ukristu kuliko wakristu wenyewe na nina hakika wapo Wakristu wanaoujua Uislaam kuliko mimi.. Hii ni elimu ya dini inategemea nani kati ya wasomi wawili bila kujali dini zao amesoma na kuelewa elimu ya dini X au Y. maana siku zote translated script are not divine scriptures. Kumbuka tu mkuu wangu mtu hungia ktk dini baada ya kukubali mafundisho ya dini hiyo kuwa ndio mwongozo bora wa maisha yake. Sii lazima awe ameelimika kujiunga na dini au dhehebu fulani..Kwa lugha nyingine tunasema kwamba sii kila msafiri ndani ya bus anajua kuendesha bus au sii kila dereva anajua Umakanika..

Kifupi kuna tofauti kubwa ya kuelewa kwa watu ktk imani za dini/Elimu..Mojawapo na kubwa zaidi ni UJINGA na nini la kufanya kuondokana na Ujinga.
Wapo watu wanajiunga na dini/shule kama njia ya kuondokana na Ujinga (kuokoka)badala ya kujifunza, kuelimika ni kuelewa ili kuondokana na Ujinga!

Sijui ka aumenipata!
 
Last edited:
kuanzia waraka wa katoliki na huu wa waislamu.
inaonesha jinsi gani tunavyotafuta golden chance ya kutibua amani yetu.

nawaambia maneno yangu kwamba tusipokuwa makini hii ngoma ambayo mwanzo wake ni lele itapata wachezaji kupitia dini. na ikianza kuchezwa itakuwa chamchela
 
Waraka wa waislamu umejikita katika unyonge wa waislamu badala ya kutoa ufafanuzi nini kifanyike ili waislamu na jamii ya watanzania waweze kujikwamua katika lindi la umaskini.Nilijua viongozi wengi wa kiislamu wamefilisika kiakili na wangetoa pumba zao kama kawaida.

Mungu ainusuru Tanzania iondokane na viongozi muflisi kama hawa wa kiislamu.
 
Makamba ni mnafiki
Lipumba ni mnafiki
Kingunge ni mnafiki
Kikwete ni mnafiki
Mafisadi ni wanafiki
Shein ni mnafiki

Mnataka waraka wa waislamu wa nini sasa, wakati nukuu chache za mashee zinatosha kuelezea walichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…