BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

Mkandara,
Lazima ukubali kwamba Waislamu wanatakiwa kuwa na chombo kimoja cha kuwaunganisha, yaani structure fulani ili serikali ikitaka kuwasiliana na waislamu ijue imuendee nani na kuongea naye. Ndivyo ilivyo kwa wakristo. Wao wana vyombo vyao, kama vile TEC na CCT. Serikali ikitaka kuwasiliana na wakristo inaenda kwenye vyombo hivi na kupata maoni yao au misimamo yao katika masuala mbalimbali.

Kwenu waislamu chombo kinachofahamika na serikali ni Bakwata. Sasa kama hamuitaki Bakwata basi muioneshe serikali mnataka chombo gani cha kuwawakilisha kama waislamu. Na hili ni jambo la lazima kwa kweli. Si kwamba kila muislamu atajitokeza tu na kusema yeye anawakilisha waislamu. Haiwezekani. Shida iliyoko kwa waislamu ni kukosa umoja katika jambo hili. Kila kikundi kinataka kiwe msemaji wa waislamu na kiwe na nguvu ya juu. Hii inaleta anarchy. Mkae pamoja na kuamua chombo gani kiwawakilishe ninyi nyote. Sidhani kama mkiamua wote kwa pamoja kwamba "chombo chetu ni hiki" serikali itakataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…