Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Mtwara Mjini limetoa tamko na kuomba dua kwa Rais John Magufuli.
Tamko walilotoa ni kumuunga mkono achaguliwe kuwa Rais kwa awamu nyingine ili aweze kuiongoza nchi.
Tamko hilo limetolewa jana na Katibu wa Bakwata Wilaya ya Mtwara mjini, Hassani Mpwago wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Danstan Kyobya, kikao ambacho kimefanyika kwenye ofisi hizo za Bakwata Mjini humo lengo likiwa ni kuweza kutambuana kati ya mkuu huyo na baraza hilo.
"Kikao hiki cha halmashauri ya Bakwata wilaya ya Mtwara mjini, tamko letu kwenye kikao hiki rasmi cha makaribisho yako tunamuunga mkono Rais John Magufuli awe amechaguliwa na aweze kuiongoza nchi yetu hatuna aibu na wala hatuna haya," alisema.
"Na tunamuombea kupitia kikao hiki tunamwombea dua maalumu na tunaomba tufikishie salamu zetu hizi kuwa Bakwata inamuombea dua njema na heri katika kampeni zake na tunaahidi kwenye baraza letu hili kura zetu zote tatampa yeye na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu awe tena Rais kwa awamu nyingine".
Hata hivyo, baraza hilo katika kutekeleza majukumu yake limekuwa likitoa usuluhishi mbalimbali ya migogoro ya kidini ikiwemo migogoro ya ndoa, talaka pamoja na mirathi ambapo kati ya mwaka 2019 hadi 2020 tayari wameshasuluhisha migogoro 88 ya ndoa na kuipatia ufumbuzi, mirathi mitano na misikiti minne.
Mbali na hayo Bakwata inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo ukosefu wa mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao kutoka ngazi zao za juu pamoja na vitendea kazi kama vile kompyuta.
Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya amesisitiza suala zima la kuzidi kudumisha ushirikiano baina yao ili kuwezesha kutatua changamoto zilizopo katika manispaa hiyo.
Mkuu huyo ameliomba baraza hilo kusimamia suala la imani katika maeneo yote kupitia nafasi yao huku akipongeza kazi za maendeleo ambayo Bakwata limekuwa likifanya kwenye manispaa hiyo kwa ajili ya kuleta ufanisi wa halmashauri hiyo.
Chanzo: HabariLeo