viongozi wa dini zetu wameanza ziara za kutembelea vyama vya siasa wakiwa na ujumbe wa amani na wakubaliane na kuvitaka vyama vikubaliane na matokeo ya uchaguzi,rai yangu ni hao viongozi wetu wa dini wajue kukubali matokeo ni matokeo ya kuwepo na uwanja huru wa ushindani wa kisiasa,naomba wakimalizana na ziara ya vyama vya siasa waende kwa msajili wa vyama ndg tendwa na wamkemee na kauli zake utata na zinazoashiria uwezokano wa uvunjifu wa amani,kisha waende kwa jaji makame na ofisi yake wanaokaa kimya huku mgombea wa chama tawala akivunja sheria ya uchaguzi huku wao wakiwa kimya,kwa kufanya hivyo hao viongozi wa dini watakuwa wamelisaidia taifa