#COVID19 BAKWATA: Waliochanjwa UVIKO-19 mwaka mmoja au miaka miwili iliyopita hawataruhusiwa hijja hadi watakaporudia kuchanja

#COVID19 BAKWATA: Waliochanjwa UVIKO-19 mwaka mmoja au miaka miwili iliyopita hawataruhusiwa hijja hadi watakaporudia kuchanja

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema waliochanjwa chanjo ya Uviko-19 mwaka mmoja au miaka miwili iliyopita hawataruhusiwa kwenda hijja hadi watakaporudia kuchanja chanjo hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Juni 24,2022 na Mkurugenzi wa Hija wa Bakwata, Alhaj Haidari Kambwili, katika semina ya mahujaji inayofanyika ofisi za Makao Makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya wahusika kwenda nchini Saudi Arabia kuhiji.

Kwenda kuhiji katika mji Makka uliopo nchini Saudi Arabia kwa mwenye uwezo ni moja kati ya nguzo tano za uislamu.

Kambwili amesema miongoni mwa masharti wanayopaswa kuyafuata wanaotaka kwenda hija ni kuchanja saa 72 kabla ya kuanza safari.

Kambwili amesema utaratibu huo wameelekezwa na nchi ya Saud Arabia ikiwa ni mkakati endelevu wa nchi hiyo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19.

Chanzo: Mwananchi
 
Duu mabeberu huwa hayana ushirika wa kudumu.
 
Ila kuna vitu vimejificha Nyuma ya hii Chanjo
 
Ila kuna vitu vimejificha Nyuma ya hii Chanjo
Kifupi akufukuzaye hakwambii toka
Saudi Arabia hawataki mahujaji toka Tanzania hata kama mtu umechanja single dose ya Johnson and Johnson

Bakwata jiongezeni mnataka hadi muambiwe watanzania hamtakiwi hija?
Hakuna maulamaa Bakwata na nje ya Bakwata na wanazuoni wa kiislamu wabobezi ndani na nje ya Bakwata kujua katazo hilo lamaanisha nini? Wawaambie mahujaji watarajiwa?
 
Hii dose ya chanjo haina kipimo cha mwishoo.

Yaani unachanja na unaambiwa urudie kirahis rahis tu
 
How does this relate with politics
Because covid 19 vaccination is nothing but political vaccination! It has no any medical value! there is no any difference in medical terms between the vaccinated and non vaccinated! The difference is enforced by political resolutions as those announced by Bakwata!! They are enforcing a vaccine market!
Hivi nani humu anaweza kutoa pesa zake hata kama ni buku kumi tu kwa ajili ya kununulia chanjo kama ingekuwa inauzwa? Hakuna hatari yoyote ya kutokuchanjwa kwa hiyo wanalazimisha ili mataifa yaendelee kuagiza chanjo zilizododa!!
 
Huko mnakokimbilia kuhiji kwanin Msiombe huyo Mungu wenu aondoke Covid19?[emoji28][emoji28][emoji28] ama covid ina nguvu kulko Mungu wenu?

Hapa ndipo watu wa dini hupaniki na kutukana matusi, ama kweli covid imeumbua upuuzi mwingi, ikiwepo upuuzi wa haya matapeli mananii hakuna hata mmoja anaeponya hili gonjwa, kumaanisha Miungu yao imepiga salute kwa covid[emoji23][emoji23].

Dini zote ni uzushi na utapeli
 
Kifupi akufukuzaye hakwambii toka
Saudi Arabia hawataki mahujaji toka Tanzania hata kama mtu umechanja single dose ya Johnson and Johnson

Bakwata jiongezeni mnataka hadi muambiwe watanzania hamtakiwi hija?
Hakuna maulamaa Bakwata na nje ya Bakwata na wanazuoni wa kiislamu wabobezi ndani na nje ya Bakwata kujua katazo hilo lamaanisha nini? Wawaambie mahujaji watarajiwa?

Mkuu - kinachotakiwa hapa no booster vaccine. Chanjo zote baada ya miezi 12 utendaji (efficacy) inakwenda chini ya 60% na maana yake mtu anaweza kuambukizwa na akaumwa na hata kufa!

Hapa ni swala la uchaguzi tu - usichanje na ubaki. Utake kwenda, pata booster shots!!

Ni nafasi nyingine ya wapinga chanjo kupata airtime. Mara hii mtuambie matokeo ya tafiti zenu za watu kufa baada ya chanjo, damu kwenye ubongo, kuwa zombie, kutoweza kupata mimba nk! Msipinge booster shots bila theories!!
 
Anyway mimi sio mtaalamu wa chanjo ma doctors jamii forums njooni huku chanjo.ya Johnson and Johnson inahitaji booster?
 
Mkuu - kinachotakiwa hapa no booster vaccine. Chanjo zote baada ya miezi 12 utendaji (efficacy) inakwenda chini ya 60% na maana yake mtu anaweza kuambukizwa na akaumwa na hata kufa!
Sio kweli mbona chanjo ya ndui unachanja mara moja tu na inadumu maisha yote
Ziko hata za ugonjwa wa manjano nk mbona hukaa miaka kibao
 
Hapo sasa Johnson and Johnson ni single dose ya Covid 19

Bakwata njooni mjibu huku
Wataalamu wa nje kama Dr Fauci wa marekani alisema hata waliochanja J&J wanaweza wakachanja chanjo zingine za Pfizer au Moderna kwa ajili ya Booster !! Lakini wataalamu wetu ndio sijawasikia kuhusu hii issue !! Tafadhali wajitokeze ili tukapate hizo booster !! Sisi wengine chanjo chanjo huwa hatuziogopi tunaogopaga vita tu kama vya UKRAINE maana vinatupandishia bei mahitaji yetu muhimu ya kila siku !!
 
Back
Top Bottom