BAKWATA watangaza Iddi ya kuchinja kuwa Juni 17, 2024

BAKWATA watangaza Iddi ya kuchinja kuwa Juni 17, 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limesema Sikukuu ya Eid el Adh’haa itakuwa Jumatatu Juni 17 na swala yake itaswaliwa katika msikiti wa Mohamed VI uliopo makao makuu ya baraza hilo Kinondoni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 8, 2024 na Katibu Mkuu wa Bakwata, Alhaji Nuhu Mruma swala ya Eid itaanza saa moja asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika pia katika msikiti huo.

“Kwa niaba ya Bakwata, Mufti na Sheikh mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir anawatakia maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” amesema Alhaj Mruma katika taarifa hiyo.

Eid El Adh’haa ni sikukuu inayoadhimishwa baada ya waumini wa Kiislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za dini.
 
Huko wanaposimama Arafa kwenyewe ambao tupo muda mmoja na Tanzania(Hatutofautiani Masaa) wao wanasimama Tarehe 15 kisha Eid al Adha ni tarehe 16.

Lakini huku Tandale maana yake tuna Arafa yetu tarehe 16 na sijui inasimamiwa wapi😃.

Ila BAKWATA 🙌🏽
 
Back
Top Bottom