The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini Tanzania, Sheikh Issa Ponda, pamoja na viongozi wengine 11 wa Kiislam, wamefungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakipinga mamlaka ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) juu ya maamuzi yanayohusu masuala ya dini.
Akizungumza kuhusu kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 13 Novemba 2024, Sheikh Ponda amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na athari kubwa zinazodaiwa kusababishwa na BAKWATA ndani ya Uislamu. Viongozi hao wanadai kuwa baraza hilo limewanyima Waislamu uhuru wa kujiamulia mambo yao, ikiwemo kumiliki rasilimali na kuendesha miradi ya kiuchumi.
"Tumeona ni muhimu kulikabili jambo hili kisheria kwa sababu ni suala linalovunja Katiba ya nchi," alieleza Sheikh Ponda. Katiba ya Tanzania inatoa uhuru wa kuabudu na kuchagua, na kwa mujibu wake, BAKWATA imekuwa ikivuruga haki hizo kwa kuhodhi maamuzi yote ya kidini kwa Waislamu nchini.
Sheikh Ponda amesisitiza kuwa lengo la kesi hiyo ni kuhakikisha Waislamu wanapata fursa ya kujiwekea uongozi wao, kusimamia rasilimali zao, na kuendesha miradi bila kuingiliwa na taasisi nyingine ambazo hazina ridhaa ya jamii ya Kiislamu.
Chanzo: Jambo TV