Uchaguzi 2020 BAKWATA yakaa kikao cha dharura, yakemea viongozi wake kupiga kampeni na Dua kinyume na Uislam. Kuwachukulia hatua

Uchaguzi 2020 BAKWATA yakaa kikao cha dharura, yakemea viongozi wake kupiga kampeni na Dua kinyume na Uislam. Kuwachukulia hatua

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo Oktoba 15, Baraza Kuu la Ulamaa BAKWATA Taifa limeketi kikao cha dharura na limetoa nasaha na maelekezo matano. Sehemu kubwa ya tamko hilo ni juu ya mienendo ya viongozi wake hasa kipindi hiki cha kampeni.

Miongoni ni kukemea Dua zinazofanywa kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislam na kutaka kauli na Dua itakayofanywa na kiongozi yeyote wa Baraza kinyume na mafundisho kamwe isihusishwe na Baraza.

Pia limewataka viongozi wake kutofanya kampeni kwa chama chochote cha siasa. Mwisho limesema linafatilia mienendo ya viongozi wake na watachukua hatua za kinidhamu watakaokwenda kinyume.

Wiki hii Sheikh wa mkoa wa Dar es Saalam alifanya kampeni kwenye moja ya mkutano wa wagombea Urais na kuomba Dua ambayo inasemwa kuwa kinyume na mafundisho ya Dini ya Kiislam.

PIA, SOMA:

Masheikh wa BAKWATA waanza kumpigia Kampeni waziwazi bila aibu




Bakwata 1.jpg

Bakwata 2.jpg
 
Kmmk wachumia tumbo
Ingekuwa taasisi hii inapigiwa kura basi tungekuwa tuisha itoa hatuipendi ss waislam wengi imekaa kama genge lawenyenjaa kupitiliza kama ingekuwa iposafi mashehe wasingeteseka hadi lisu mkatoliki roho inamuuma kweli wao wapo namagari yakifahari kilamkutano wamkuu wapo vyote nivyakubaki umeindaa ahera?
 
Back
Top Bottom