BAKWATA yalaani vikali tukio kushambuliwa Katibu wa TEC Padri Charles Kitima

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katibu Mkuu BAKWATA Alhaj Nuhu Jabir Mruma amesema Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), linalaani vikali tukio lililotokea jana la kushambuliwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kwa mujibu wa taarifa maalum aliyoitoa leo Alhamisi jioni Alhaj Mruma amevitaka vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi wa kina na haraka na kuwachukulia hatua watakaobainika kufanya shambulio hilo

Kwenye taarifa hiyo, Alhaj Mruma ametoa rai kwa Waislamu na Watanzania kwa ujumla, kuendelea kuwa na subira wakati vyombo vikiendelea na uchunguzi.

Soma Pia: Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Alhaj Mruma amesema BAKWATA na Mh. Mufti kwa ujumla linamtaka kila Mtanzania popote alipo kuwa Balozi wa Amani na kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi yetu, amani ambayo ni tunu ya taifa letu.

Katibu wa TEC Padri Charles Kitima alishambuliwa jana Jumatano usiku Kurasini jijini Dar es salaam.

 

Okay sawa.

Lakini BAKWATA waache mtindo wao wa kujibu Hoja zenye malengo chanya ya kudai HAKI za kijamii na za kiraia kwa kuchomekea Hoja zao za Udini.
Mada au Hoja zinazohusu Haki za binadamu ni lazima zitenganishwe na masuala ya udini.
 
Wamlaani na Samia kwa kutesa, kuumiza na Kuua watu wanaodai mabadiliko.
 
takataka, tawi la CCM , nao ni washiriki wa mauaji haya maana silence means consent!
 
Hiyo Taarifa ipo wapi
 
Ila yule Shekhe wa Mei mosi alikuwa kiboko 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…