Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuberi ameshangazwa na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kutokemewa lakini badala yake wanalindwa na kutafutiwa uhalali wa ndoa akiwataka Watanzania wote kulaani na kukataa ndoa za jinsia moja nchini. Mufti alitoa hadithi ya nabii Lut ambapo jamii yake ilishiriki vitendo vya jinsia moja na miji yao kupinduliwa juu chini.
Mufti amesikitishwa na wanaume kuingilia wanaume wenzao ilhali wanawake wapo akidai ni muujiza mkubwa watu hao leo kupewa nafasi na kuwa huru ikionekana jambo la kawaida. Mufti anasema si sawa vitendo hivyo kufundishwa mashuleni.