Balaa la walimu waliozaliwa mwaka ya 1980

Balaa la walimu waliozaliwa mwaka ya 1980

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Ualimu ni taaluma inayotaka nidhamu na maadili ya hali ya juu. Hilo ni kwa kuwa ndio taaluma inayohusiana moja kwa moja na malezi ya watoto.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kada hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimball, Ikiwamo utovu wa maadili na ukengeukaji wa miiko miongoni mwa walimu.

Matukio kama vile walimu kuwa na uhusiano na wanafunzi wao, ulevi na hasira kubwa kwa wanafunzi wanapowarudi, sio mageni nchini, na bila shaka yanaeka doa katika taaaluma hiyo nyeti na adhimu.

Taarifa za Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) zinaonyesha tangu mwaka 2016, tume hiyo imepokea mashauri ya kinidhamu 11,396 yakiwahusu walimu 7579.

Makosa waliyokutwa nayo ni pamoja na kughushi vyetu mashauri 1438 (sawa na asilimia 33.5), uhusiano wa kimapenzi mashauri 328, ulevi 89 na uzembe kazini mashauri 56.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamishna wa TSC, Mariam Mwanilwa, walimu waliozaliwa kati ya mwaka 1980 hadi 1988, wameonekana kuwa vinara wa mashauri hayo kuliko rika jingine katika kada hiyo ya ualimu.

"Kwa kuangalia takwimu hizo, ufanyike utafiti kuangalia aina ya makosa, umri na jinsi ambayo walimu wamekuwa wakituhumiwa


IMG_8862.jpeg
 
Back
Top Bottom