Mucadama ni kweli kwamba Balabouh alifikishwa mahakama ya kisutu jana kuungana na wale washitakiwa saba wengine.lakini alipata dhamana na yuko nje kwa dhamana. Nilijua mapema kwamba Balabouh naye angefikishwa mahakamani lakini nisichofahamu ni kwanini alichelewa kuunganishwa katika kesi hii wakati ushahidi ulikuwa wazi kwasababu yeye ndiye mmiliki wa Kigamboni Oil Company ambako mchezo wote wa ule wizi wa $1million ulikoanzia.
Mwakilishi wa Kigamboni bwana Ukwaju ambaye ndiye aliyekuwa anaenda kuchota pesa kule alishaunganishwa katika kesi muda mrefu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.