Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Walinda legacy wamechachamaa! 😁😁😁

Magufuli alikuwa anakopa utadhani hakuna kesho!

Aina ya mikopo aliyokuwa akichukua Magufuli siyo ya masharti nafuu ni kitanzi kitupu!
Nahisi unaamini mkopo wa serikali ni kama kukopa kwa mpemba. Mikopo ya serikali ina vigezo. Nchi inachunguzwa na hata mradi unachunguzwa. Ukiona unakopeshwa, fahamu unakubalika. Wanaokopesha siyo failed state, ni nchi na taasisi zinazojitambua. Sasa wewe kama unazomea-zomea kutafuta ushindi kama kwenye Ndondo cup, ni ufahamu mdogo.
 
Ni rahisi kusema hayo, lakini ni kukumbushe tu kuwa si yote unayoyaona yanaonekana leo yalikuwepo katika awamu ya 5. Nikiyataja hayo maswala ni mengi kwa mfano: Mahakama kimsingi ni chombo kilicho huru na hakipaswi kuingiliwa na serikali lakini sidhani kama katika awamu ile Sabaya angeweza kufikishwa mahakamani. Wala sidhanikama mengi yanayoandikwa sasa hivi katika hizo Tovuti za wizara, maudhui yenye ubora huo ungeandikwa wakati wa awamu ya 5.

Fikiria mwenyewe kama serikali ya awamu ya 5 ilikopa pesa hizo kwa ajili ya miradi, zile kelele zilizopigwa kuwa tunajenga kwa fedha yetu wenyewe ni kweli au magumashi. Na kama ni kweli, hizo pesa tulizokopa zimeenda wapi au kinyume chake , yaani kama tumejenga miradi kwa fedha za kukopa hizo pesa zetu za ndani zimekwenda wapi na ni kiasi gani.

Na nijulishe tovuti nitayopata mjumuisho wa fedha hizo (mkopo kiasi gani na fedha za ndani zilizotumika ktk miradi ni kiasi gani) na matumizi yake.
 
ujinga huu
 
THREAD OF THE YEAR. Penda usipende lakini huu ndio ukweli. Thread imejaa takwimu, ufafanuzi, majumuisho na hitimisho nzuri sana.

Like zaidi ya 60, kurasa zinapepea tu na zimeshafika zaidi ya 25 na bado kalamu zinaendelea kuandika.

Mengi yatakuja kuhusu awamu ya 5, mazuri na mabaya. Mizani unayo wewe msomaji au mwananchi.
 
Si bora alijenga hiyo miradi na value for money ikaonekana. Kuliko angekopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Sasa kwa nini alidanganya alijenga kwa hela za ndani? Lilidhani litaishi milele na urais. Matrilion ya Watanzania aliyoiba na kuchezea ameyaacha. Matokeo yake analambushwa makofi ya moto huko kuzimu.
 
Huu ni utumbo kutolewa mtu anayetegemewa katika jamii na naweza kusema rushwa imerudi na mambo yale ya media na watu maarufu kuhongwa kuleta mijadala ya kisiasa kusaidia wanasiasa imerudi... Balile hutakiwi kuangalia serikali inakopa au inakopa kiasi gani ungekuja na hoja ya serikali imekopa kiasi gani kwa mambo ambayo ni ya hovyo...mfano tumekopa fedha imeishia kwenye semina warsha na safari zisizo na tija hapo nitakusikiliza...lakini kulinganisha mikopo ya serikali iliyopita bila kulinganisha na miradi mikubwa ya kimkakati na miradi katika sekta zote then hutapata shida ya kujua kwanini mikopo inaongezeka...tusitishane kwenye kukopa au kuwa na madeni bali tuwe wakali katika kutumia hiyo mikopo vizuri ili wakati tunarejesha tija ya mikopo inaonekana.dont force to have short mind for kick back.
 
Nashangaa wachangiaji hapa, wameanza kumshutumu Balile!
Ulichokiandika hiki mkuu, ndiyo hoja kuu. Watetezi, wajikite kwenye hoja hii!
mboni umeiacha "yeye kusababisha Rais kuapishwa !?..jf raha
 
Linaendana na idadi ya miladi na thamani yake au kubance equation haujui?
 
swali zuli mkishapata thamani ya miladi mtupe na taarifa zamakusanyo ya kodi zilizokusanywa kwakuvuka malengo kila mwezi zilikuwa zinafanya nini?
 
Hizo propaganda ziliharibu sana vijana mpaka leo wengine bado wanaweweseka.
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
 
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
Yaani wewe na kundi lile mlijiona mnajua kunyumbulisha maneno ya hadaa kwa wananchi mliowabatiza jina la wanyonge ili mfisidi vizuri bila kubugudhiwa.

Mlisema miradi inajengwa kwa "fedha zetu za ndani" Je mikopo hiyo iliyofikisha deni la tr 78 ilitoka taasisi au mkoa gani wa tanzania?

Kama umekwenda kukopa nje ya nchi, je neno "fedha zetu za ndani" hauoni kuwa linapoteza maana?

Unapokopa fedha au mali yoyote haiwezi kuwa yako kwa %100 Hadi utakapomaliza deni hilo vinginevyo muda wowote unaweza kupokonywa mali hiyo.

Acha kuendelea kutetea utapeli wa hadaa kwa mliowaitwa wanyonge ambao mliwageuza kuwa ngao yenu ya kupiga hela na kuligharimu taifa.
 
Hebu tujikumbushe kidogo hapa gazeti la jamhuri liliwahi kunene
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…