Balile: Usalama wa Kidigitali ni muhimu kuangaziwa dira 2050

Balile: Usalama wa Kidigitali ni muhimu kuangaziwa dira 2050

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameitaka serikali kutoa nafasi zaidi kwa vyombo vya habari kama sehemu ya kichocheo muhimu cha kuhakikisha malengo na mipango ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inatekelezwa kikamilifu ndani ya muda uliopangwa, lakini pia kuzingatia masuala mazima ya usalama na ulinzi wa kimitandao katika wakati huu ambao kuna mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia.

Balile ameyazungumza hayo katika Mkutano wa Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatatu Desemba 16, 2024.

"Kwenye vichocheo tumeacha jambo la msingi sana, vyombo vya habari. Ile dira ya kwanza iliacha vyombo vya habari, ukiona sasa hivi tunasema tunataka kuhifadhi utamaduni wa Mtanzania, tuviweke vyombo vya habari ili visaidie kubeba haya mahudhui, tuweke mpango kwamba tunapeleka utamaduni wa Tanzania." Amesema Balile.

Katika hatua nyingine, Balile pia amesisitiza umuhimu ulinzi na usalama kupewa kipaumbele zaidi katika kuendana na mabadiliko mbalimbali ya kidijiti yanayoshuhudiwa kote duniani pamoja na matumizi makubwa ya teknolojia katika ulinzi na usalama.
 
Back
Top Bottom