BALLON D'Or IMPELEKE EDEN HAZARD HISPANIA?

BALLON D'Or IMPELEKE EDEN HAZARD HISPANIA?

8th President

New Member
Joined
Oct 15, 2018
Posts
2
Reaction score
2
8th President

Eden Michael Hazard alizaliwa tarehe 07-January 1991,ni mchezaji wa Chelsea Fc na timu ya taifa ya Ubelgiji.
Uwezo wa Hazard kukokota mpira,Ubunifu & kasi vimemfanya kufananishwa na washindi wa Ballon d'Or Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Haina ubishi Eden Hazard ni moja ya wachezaji bora kabisa kwa sasa juu ya sayari hii na hivi karibuni alinukuliwa akisema anahitaji kwenda Hispania ili ashinde Ballon d'Or.

KWANINI HASA HAZARD ANATAKA KWENDA HISPANIA.

Ballon d'Or pengine moja ya tuzo kongwe kabisa ulimwenguni katika soka ilianza kutolewa rasmi na jarida la Ufaransa la Ballon d'Or mwaka 1956,kila mchezaji ana ndoto za kutwaa tuzo hii katika maisha yake ya soka.Lakini tujiulize ni sababu gani hasa ya msingi inampeleka Hazard Madrid.
Kwanza tuanze kuziangazia tuzo kubwa za Ballon d'Or na zile za FIFA:

TAKWIMU MUHIMU KUIHUSU BALLON D'OR.

*Tuzo hii hadi sasa imetolewa Mara 57 na katika Mara zote hizo wachezaji kutoka Hispania wametwaa tuzo hii Mara 21,karibia nusu ya tuzo zote.

*Wachezaji kutoka England wametwaa Mara 5 pekee.

FIFA WORLD PLAYER OF THE YEAR.
Hii ni tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia iliyoanza kutolewa rasmi mwaka 1991.

TAKWIMU MUHIMU KUHUSU TUZO YA MWAKA YA FIFA

Tuzo hii imetolewa mara 28 huku wachezaji kutoka Hispania wakiitwaa Mara 19,zaidi ya Mara nusu ya Mara zote.

*Wachezaji kutoka England wametwaa Mara moja pekee.

Kutoka na takwimu hapo juu kuzihusu tuzo hizo kubwa,binafsi siku zote ninaamini ligi kuu ya Hispania na soka la Hispania ni bora sana kwa muda wote ukilinganisha na like la England,Mpira wa hali juu unapatikana Hispania,Wachezaji bora kabisa duniani wamecheza katika ligi hii,Bila ubishi ni ligi bora kabisa.

-Umuhimu wa Hazard kuelekea katika ligi kuu ya Hispania kama yeye alivyonukuliwa akisema ni mkubwa sana hasa ikizingatiwa klabu za Real Madrid & FC Barcelona muda mwingi zinashiriki katika michuano mikubwa hasa ile ya ligi ya Mabingwa Ulaya tofauti na klabu ya Chelsea anayochezea sasa.

TAHADHARI KWA HAZARD.

Hazard ni mchezaji wa kiwango cha juu sana lakini changamoto kubwa kwa Hazard ni uwezo wa kufunga.

Ukilinganisha takwimu za Hazard na wachezaji wa eneo lake kama Leonel Messi,Ronaldo,Neymar Jr na hata Mbappe,wana takwimu nzuri za ufungaji kuliko Hazard,ili uwe bora katika eneo analocheza Hazard kwa mpira wa kisasa ni lazima uwe na takwimu nzuri za kufunga magoli.

Pili,japokua ni kweli takwimu zinawabeba Wachezaji kutoka Hispania katika tuzo hizi kubwa,lakini Hazard anatakiwa kusoma alama za nyakati.

Kwa sasa Hazard anajijengea Ufalme,si Chelsea na London pekee lakini ni England, ndiye mchezaji bora kabisa aliyebaki,cha kujivunia ni kuwa Hazard ametwaa mataji yote England na Ulaya isipokua Ligi ya mabingwa pekee na Chelsea wanampa heshina anayostahili na pia wako tayari kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi England na pengine ulimwenguni.

Upande wa pili,Real Madrid ni klabu bora ulimwenguni hili halina ubishi,lakini haimaanishi kuwa haina vipindi vya mpito (transitional periods).

Wachezaji kama Arjen Roben & Robinho waliwahi kujiunga na Real Madrid kwa matarajio makubwa ya kuwa wachezaji bora ulimwenguni lakini waliikuta klabu katika kipindi kigumu,misimu sita mfululizo 2004-2010,Real Madrid ilipotea kabisa usoni mwa soka la Ulaya.

Tunamkumbuka James Rodriguez, japokua aliikuta Real Madrid katika kipindi kizuri lakini bado ilimpa shida kuonesha alichonacho.
Hiyo nayo ni taa ya alamu kwa Eden Hazard.

Mwisho,Binafsi ningekua mshauri wa Eden Hazard,ningemshauri aende zake Hispania kama anataka kuwa mchezaji bora ulimwenguni na kutwaa tuzo hiyo ya Ballon d'Or,lakini kuna haja ya kusoma upepo hasa wa klabu anayoiota ya Real Madrid,kama ataona hauruhusu atulie kwanza England.
 
Aende serie A atleast ataweza kuchuana na Dybala...Spain kuna King wa soka tena asithubutu kutua pale....
 
Abaki England ataweza chukua pale pale Chelsea.
 
Back
Top Bottom