Mshambuliaji wa kiitaliano Mario Baloteli aka Super Mario jana alifunga mara mbili na kuisaidia timu yake ya Nice kukwaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kwa kufikisha alama 14 katika michezo 6. Nice inafuatiwa na PSG yenye alama 13.
Nice ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Monaco wanaoshikilia nafasi ya 3 wakiwa na alama 13. Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Riviera, Nice waliwapoteza Monaco katia kila idara. Baloteli alifunga mabao yake katika dakika za 30 na 69 za mchezo huo.