Pre GE2025 Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi: CCM Itawashinda Wapinzani Kwa Namna ambayo hawajawahi kushindwa

Pre GE2025 Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi: CCM Itawashinda Wapinzani Kwa Namna ambayo hawajawahi kushindwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa wito kwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) pamoja na jumuiya nyingine za chama hicho kuendelea kushindana kwa hoja na kuwa mfano bora wanapojadili masuala mbalimbali ya kitaifa.

Akizungumza katika hafla ya kumaliza matembezi ya vijana kuadhimisha kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Balozi Nchimbi aliweka wazi kuwa nafasi ya CCM kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Novemba inategemea sana juhudi za vijana hao.

Balozi Nchimbi, aliyekuwa akizungumza mbele ya vijana takriban 2,156 waliotembea kutoka Butiama, Mkoa wa Mara, hadi Nyamagana, Jijini Mwanza, alisisitiza umuhimu wa vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele katika kutafuta kura kwa bidii.

Alieleza kuwa ushindi wa CCM hautapatikana kwa kubahatisha, bali kwa juhudi za makusudi na mipango ya kimkakati, huku akiwataka vijana hao kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa.

“Vijana wa UVCCM, ninyi ni nguzo muhimu katika chama hiki. Ushindi wa CCM uko mikononi mwenu. Mnapaswa kushindana kwa hoja na kuhakikisha mnatafuta kura za CCM usiku na mchana. Tunataka ushindi wa aina ambayo wapinzani wetu hawajawahi kushindwa tangu chaguzi hizi zianze. Na baada ya hapo, tutawashukuru kwa ushiriki wao mzuri kwenye mchakato wa uchaguzi,” alisema Balozi Nchimbi.

Soma Pia: Dkt. Nchimbi: Acheni kupanga safu, viongozi bora ndio wapitishwe, ni kosa kubwa la kimaadili kiongozi kumkamia mwanachama kwamba atahakikisha anakatwa

Pamoja na kutoa wito huo kwa vijana, Nchimbi alitoa pongezi kwa UVCCM kwa kuandaa matembezi hayo, ambayo alisema yamekuwa na maana kubwa kwa Chama na Taifa zima.

Alieleza kuwa matembezi ya vijana yaliyoanza tarehe 9 Oktoba 2024 hadi 13 Oktoba 2024, yameleta faraja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.

Alisema Rais Samia ni muumini wa falsafa za Mwalimu Nyerere, na hivyo matembezi hayo yamemgusa kwa namna ya kipekee.

“Nimefurahi sana kuona vijana wa UVCCM mmekuwa na ujasiri wa kuandaa matembezi haya. Mwalimu Nyerere alikuwa mfuasi wa falsafa zake mwenyewe, na mara ya kwanza alitembea kwa miguu kuunga mkono Azimio la Arusha. Kuanzia hapo, matembezi ya miguu yamekuwa ishara ya imani thabiti kwa jambo fulani. Kwa hatua hii, UVCCM mmefanya jambo kubwa sana ambalo limeleta faraja kwa Rais Samia na kwa wote tunaopenda historia ya nchi hii,” aliongeza.

Aidha, Balozi Nchimbi alisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, Muungano wa Tanzania umekuwa na ustawi mkubwa, na amani imeendelea kudumu.

Alisema ni jukumu la vijana kuendeleza falsafa za Baba wa Taifa na kuhakikisha wanaendeleza mshikamano ndani ya chama na katika jamii kwa ujumla.

Katika ujumbe wake wa mwisho, aliwataka vijana hao kuzingatia wajibu wao wa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Alisema kwa jitihada na ushirikiano kati ya vijana na wazee wa chama, ushindi wa chama hicho utakuwa wa kihistoria na wa kipekee.

“CCM ni chama cha wazee na vijana. Wazee ndio waanzilishi wa chama, lakini sasa nyinyi vijana ndio mna jukumu la kuhakikisha chama kinaendelea kushinda. Lazima tushirikiane kwa karibu kuhakikisha tunaleta ushindi mkubwa wa CCM kwenye uchaguzi huu ujao. Nina uhakika tutaweza kufanya hivyo,” alihitimisha Balozi Nchimbi.
Screenshot_20241013-215609_1.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20241013-215609_1.jpg
    Screenshot_20241013-215609_1.jpg
    191.8 KB · Views: 2
Tangu kuanza uchaguzi unaohusisha vyama vingi mwaka 1995 kwa mwaka huu na mwakani tutakuwa na upinzani dhaifu mno kupata kutokea. Kwa mara ya kwanza katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani anakilaumu CCM kutohamasisha wanachadema kujiandikisha kupiga kura. Inasikitisha sana. Hata huko Marekani kina Trump kama wapinzani wanahimiza wanachama wao kujiandikisha ila hapa kwetu upinzani unawalaumu CCM kwa majukumu yao. Inakera mno uchaguzi kuwa na upinzani dhaifu kiasi hiki.
 
Ni lazima CCM iibuke na ushindi wa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
Katibu mkuu hajui kuwa wapinzani hawana hoja zaidi ya matusi? UVCCM watakuwa wana kazi rahisi mno dhidi ya hawa watu wanaodhani matusi ni sera. Mimi ninadhani CCM ingeanza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya 2025 kama ipo tayari kwasababu ushindi ni lazima wa kishindo.
 
Katibu mkuu hajui kuwa wapinzani hawana hoja zaidi ya matusi? UVCCM watakuwa wana kazi rahisi mno dhidi ya hawa watu wanaodhani matusi ni sera. Mimi ninadhani CCM ingeanza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya 2025 kama ipo tayari kwasababu ushindi ni lazima wa kishindo.
Ccm imeshapoteza uwezo wa kushindana kwa hoja, ndio maana tunashuhudia chaguzi za kishenzi mno ili ccm watangazwe washindi.
 
Nchimbi yuko sahihi! CCM itashibda kwasabb mifumo ya uchaguzi imejaa wizi na ubabe. CCM ni refa na ndiyo mchezaji, unategemea nini?
CCM itashinda kwa sababu inaaminika kwa watanzania kutokana na kufanya kazi kubwa zinazogusa maisha ya watu.pamoja na kuwa na sera na ajenda zenye kugusa watu wa makundi mbalimbali
 
Ccm imeshapoteza uwezo wa kushindana kwa hoja, ndio maana tunashuhudia chaguzi za kishenzi mno ili ccm watangazwe washindi.
Hakuna chama chenye uwezo wa kushindana na CCM iwe ni jukwaani au katika sanduku la kura
 
Nchimbi yuko sahihi! CCM itashibda kwasabb mifumo ya uchaguzi imejaa wizi na ubabe. CCM ni refa na ndiyo mchezaji, unategemea nini?
Kama wana uhakika wa ushindi, wanaogopa nini kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi? Kwa nini CCM na Rais wao hawataki tume huru ya uchaguzi, hawataki katiba nzuri mpya, wanateka na kuua wanaowakosoa?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Hakuna chama chenye uwezo wa kushindana na CCM iwe ni jukwaani au katika sanduku la kura
Mkuu unafikiri ni kwa nini Mh. Dr. Nchimbi anasisitiza kushindana kwa hoja?? Ni kwa sababu anawajua vijana wake wengi ni mweupe upstairs nawe ukiwemo!!!

Anaelewa vijana wake hawachelewi kuzua vurugu wakishindwa hoja.

Mkuu, Nchimbi ameiona hatari inayokuja kuwa sio kabisa maana mazingira yaliyopo yamefikia hatua ya ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali na kuukanyaga!!

Usione watu wapo kimya, wamefika mwisho!! Tume ya uchaguzi, polisi na mahakama hawaaniniki!!!

Masauni pale msibani alionjeshwa tu, Inahitajika cheche tu, na Nchimbi kashaona!!
 
Kama wana uhakika wa ushindi, wanaogopa nini kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi? Kwa nini CCM na Rais wao hawataki tume huru ya uchaguzi, hawataki katiba nzuri mpya, wanateka na kuua wanaowakosoa?
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka Marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
 
Kuna kanchi wizi wa kura huwaingiza viongozi wake madarakani.
Kisha bila haya fyongozi hao hushika vitabu vitakatifu na kuapa mbele za Mungu na watu woote kuwa watatenda haki....baada ya wizi...

Uthibitisho upo wazi na waliosema ukweli walifukuzwa kazi... cc. Nepi et al
 
Back
Top Bottom