Pre GE2025 Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi: CCM Itawashinda Wapinzani Kwa Namna ambayo hawajawahi kushindwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kunanchi wizi wa kura ndiyo huwaingiza viongozi madarakani kisha hushika vitabu vitakatifu kuapa mbele za Mungu na watu woote kuwa watatenda haki....baada ya wizi...

Uthibitisho upo wazi na waliosema ukweli walifukuzwa kazi... cc. Nepi et al
Kama mnajua mnaibiwa mmechukua hatua gani? acheni vilio havina msaada
 
Kama wana uhakika wa ushindi, wanaogopa nini kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi? Kwa nini CCM na Rais wao hawataki tume huru ya uchaguzi, hawataki katiba nzuri mpya, wanateka na kuua wanaowakosoa?
Kwahiyo unataka ccm wakupe tume huru ya uchaguzi?
 
Kama wana uhakika wa ushindi, wanaogopa nini kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi? Kwa nini CCM na Rais wao hawataki tume huru ya uchaguzi, hawataki katiba nzuri mpya, wanateka na kuua wanaowakosoa?
CCM wanatakiwa kuleta tume huru ya Uchaguzi kwa hiari yao ?

Wapinzani wamechoka kufanya Siasa.
 
Ni kweli, maana ccm sio chama cha siasa, bali kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa.
Utaendelea kupiga makelele yako huku CCM ikiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania
 
Kushinda kihalali sawa ila kushinda kwa kuiba kura ni aibu. Ushindani wa haki wa kisiasa utalijenga Taifa.
 
CCM wanatakiwa kuleta tume huru ya Uchaguzi kwa hiari yao ?

Wapinzani wamechoka kufanya Siasa.
Kwa style ile ya kujaza polisi wenye ma SMG na AK47 kila makutano ya barabara ili tu kudhibiti maandamano ya amani kwa chama pinzani unafikiri inaleta picha gani kwa mtu timamu?

Ni kwamba CCM inawachukulia wapinzani kwa chuki kama magaidi flani. Hawatakiwi kupumua kwa namna yeyote ile kisiasa. Halafu mtu anajitokeza kujisifu kuwa CCM itashinda kwa kishindo sana hii ni kebehi isiyomithilika. Unamfunga mtu mikono halafu unajisifu umempiga na hajajibu mashambulizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…