Marehemu atazikwa kijijini kwao Tongwe, Muheza Jumatano mchana.Jumanne jioni kutakuwa na Misa ambayo itafanyika St.Albans na baadaye kuuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake Makongo...Kwa wale watakaoenda Muheza -Tanga, safari itaanzia Makongo..kuna magari kadhaa ambayo yapo wazi kwa wanaotaka kuhudhuria Mazishi.
Serikali itawakilishwa na Waziri wa Elimu,katika mazishi hayo. Baadhi ya Watoto wa marehemu wamekwishawasili Dar-es-salaam kwa ajili ya utaratibu wa Mazishi ya Baba yao.Kama kuna chochote na Upo Dare-es-salaam usisite kuwasiliana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Vicent Mrisho) ambaye ndiye Mratibu Mkuu wa shughuli ya Msiba.
Mkuu BabaDesi kwa ufahamisho tu ni kwamba Eva amewasili mchana leo(Jumatatu) akitokea Washington Dc kwa ajili ya mazishi,na atakuwepo Dar mpaka baada ya 40.