TANZIA Balozi Emanuel Ole Naiko afariki Dunia Dar

TANZIA Balozi Emanuel Ole Naiko afariki Dunia Dar

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
20220330_171034.jpg

Familia ya Emmanuel Ole Naiko inasikitika kutangaza kifo cha BABA YAO, BALOZI EMMANUEL OLE NAIKO kilichotokea leo 30/03/22, nyumbani kwake Bahari Beach, Dar es Salaam.

Habari ziwafikie wana familia waliopo Dar es Salaam, Monduli-Arusha na kwengine kote.

Balozi Ole-Naiko amewahi kushika nyadhifa mbali mbali kwenye serikali ikiwemo Mkurugenzi mkuu wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Wakati wa mauti unamfika alikuwa ni balozi wa Heshima wa Botswana.

Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Utulivu Road, Bahari Beach, Dar es salaam

Balozi Naiko alizaliwa tarehe 24 Julai 1951.

Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

2 Timotheo 4; 7
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda
 
Hakika Mola wetu ndiye aliyetoa, na sasa pia ndiye aliyemtwaa mja wake. Jina lake na lizidi kuhimidiwa.

[emoji120]

Pole ziwafikie familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote ambao wanaguswa na msiba huu.



Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom