Balozi Innocent Shio awapokea viongozi waliowasili Ethiopia kushiriki kikao cha 46

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika na Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Innocent Shio akiwapokea viongozi waliowasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kushiriki Kikao wa 46 Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika kinachofanyika tarehe 12 na 13 Februari, 2025 na kufuatiwa na Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 15 na 16 Februari, 2025 nchini humo.

Viongozi hao waliowasili na kushiriki Kikao cha ndani cha maandalizi ya Mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Bi. Christina Mndeme

 

Attachments

  • IMG-20250212-WA0083.jpg
    365.7 KB · Views: 2
  • IMG-20250212-WA0086.jpg
    399.4 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…