Balozi Karume: Niko tayari kupokea uamuzi wowote utakaotolewa na CCM dhidi yangu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1687161377720.png

Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Abeid Karume amehojiwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho na kuweka wazi kwamba yupo tayari kupokea uamuzi wowote utakaochukuliwa dhidi yake.

Hali hiyo imefuatia baada ya kauli yake ya hivi karibuni katika moja ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii, akisema CCM kipo madarakani si kwa sababu kilishinda uchaguzi, bali kwa sababu ya uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Balozi Karume ameitwa kwenye kamati ya maadili baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar kuonya baadhi ya wanachama wa CCM kuvunja maadili na utamaduni wa chama hicho kwa kuzusha mambo ambayo yanahatarisha uhai wa CCM.

Alipoulizwa atahamia chama gani iwapo atafukuzwa CCM, amejibu kuwa hajajiandaa kufukuzwa uanachama na kama ikitokea hawezi kuhamia chama kingine chochote cha siasa, kwa sababu moyo na mapenzi yake bado yapo ndani ya CCM.

Kuhusu taarifa zilizosambaa mtandaoni akisema kadi yake ya American Express na Viza+ ni muhimu kuliko kadi ya CCM, amesema, “Ndiyo nimesema kwa sababu kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi.”
 
Hii familia nzima ya karume ni wapuuzi kabisa, kuanzia wazee mpaka watoto wao, amesahau kuwa hata baba yake alipewa Uraisi bila kufanya lolote. Mapinduzi walifanya wengine yeye akaja kupewa tu hicho kiti.
Unakosea sana kui - label familia nzima kuwa ni ya kipuuzi kwa sababu ya makosa au weakness fulani fulani za babu zao huko nyuma..!!

Mambo na mwelekeo wa mitazamo huwa unabadilika kulingana na seasons & times, ndugu. Hakuna shida yoyote Kwa hawa wa kizazi hiki kuwa na uelekeo na mtazamo tofauti..

Wewe unadhani kwa kuwa babu na baba walipewa au walikuwa wezi, basi na watoto wanaweza kuwa hivyo..??

Sometimes huwa iko hivyo. Lakini huwa haiko hivyo mara zote!

Kwa hiyo sio ajabu kabisa kuwa huyu aakuwa na mwelekeo mwingine tofauti na wazazi au babu zake...

Hata Fatuma Karume mjukuu wa Mzee Karume (Sr) ni critic mkubwa wa mfumo. She is always against mambo yaliyotendwa na babu na baba zake...!
 
kwa ujumla wote ni wafaidika wa huu mfumo, hata Fatma na yeye ni mfaidika. Na tumeona mara kwa mara watoto wa vingozi baba zao wakiachia ngazi ndio utawasikia wanaongea.
 
Hii familia nzima ya karume ni wapuuzi kabisa, kuanzia wazee mpaka watoto wao, amesahau kuwa hata baba yake alipewa Uraisi bila kufanya lolote. Mapinduzi walifanya wengine yeye akaja kupewa tu hicho kiti.
Vp famulia ya nyerere? Hao ndio wapuuzi watupu kabisa
 
kwa ujumla wote ni wafaidika wa huu mfumo, hata Fatma na yeye ni mfaidika. Na tumeona mara kwa mara watoto wa vingozi baba zao wakiachia ngazi ndio utawasikia wanaongea.
Ni kweli imetokea, inatokea sasa na pengine itatokea huko mbeleni...

Lakini kumbuka kuwa, huwa zipo sababu za kawaida na zisizo za kawaida za kutozungumza wakati ndugu zao wakiwa madarakani. Hopefully, unalielewa..

However, hoja ni ileile, kuwa kila mtu ni unique with his/her own mission & vision na kwa sababu hiyo, si lazima mtoto awe na tabia na mtazamo kama wa ndugu zake hata km ni wazazi...
 
Hii familia nzima ya karume ni wapuuzi kabisa, kuanzia wazee mpaka watoto wao, amesahau kuwa hata baba yake alipewa Uraisi bila kufanya lolote. Mapinduzi walifanya wengine yeye akaja kupewa tu hicho kiti.
Sio karume pekee!

Pale kwa nyerere unamuona kiongozi yeyote tishio kwenye siasa zetu!!?

Sijui labda kulikua na jitihada za kuhakikisha wanakua kama walivyo hivi leo!!
 
Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Abeid Karume amehojiwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho na kuweka wazi kwamba yupo tayari kupokea uamuzi wowote utakaochukuliwa dhidi yake.

Hali hiyo imefuatia baada ya kauli yake ya hivi karibuni katika moja ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii, akisema CCM kipo madarakani si kwa sababu kilishinda uchaguzi, bali kwa sababu ya uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Balozi Karume ameitwa kwenye kamati ya maadili baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar kuonya baadhi ya wanachama wa CCM kuvunja maadili na utamaduni wa chama hicho kwa kuzusha mambo ambayo yanahatarisha uhai wa CCM.

Alipoulizwa atahamia chama gani iwapo atafukuzwa CCM, amejibu kuwa hajajiandaa kufukuzwa uanachama na kama ikitokea hawezi kuhamia chama kingine chochote cha siasa, kwa sababu moyo na mapenzi yake bado yapo ndani ya CCM.

Kuhusu taarifa zilizosambaa mtandaoni akisema kadi yake ya American Express na Viza+ ni muhimu kuliko kadi ya CCM, amesema, “Ndiyo nimesema kwa sababu kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi.”
Watu wamechoka na takataka CCM
 
Back
Top Bottom