Balozi Kiplagat afariki dunia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532




Nairobi. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Maridhiano ya Kenya (TJRC), Bethuel Kiplagat amefariki. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, Kiplagat amefariki akiwa na umri wa miaka 80 katika Hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Balozi Kiplagat ambaye aliwahi kuwa mwanadiplomasia na Ofisa wa Serikali ya Kenya, alifanya kazi akiwa Mwenyekiti wa TJRC tangu mwaka 2009 hadi Novemba 2010. Alijiuzulu baada kuchunguzwa kwa jukumu lake kuhusu unyanyasaji wa haki za kibinaadamu, hususan jukumu lake katika mauaji ya Wagalla 1984.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Kiplagat alirudishwa kuiongoza tume hiyo hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa wanachama wenzake wa tume hiyo mwaka 2012.

Alifanya kazi kama mjumbe maalum wa Kenya katika mpango wa amani nchini Somalia kati ya mwaka 2003 na 2005 na kuongoza bodi ya hazina ya utafiti wa matibabu barani Afrika kutoka mwaka 1991 hadi 2003.

Awali alikuwa balozi kwa miaka 13 tangu 1978-1991 akiwa balozi wa Kenya nchini Ufaransa na katibu wa kudumu katika Wizara ya Masuala ya Nchi za Nje.



Chanzo: mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…