Balozi Mahiga: Vijana wa Tanzania ni kati ya wapiganaji wanaounda kundi la Al-Shabaab

Balozi Mahiga: Vijana wa Tanzania ni kati ya wapiganaji wanaounda kundi la Al-Shabaab

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
maiga-na-sheikh.jpg

Balozi wa Umoja wa Mataifa, Augustine Maiga, akitoa mada wakati maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yaliyojadili Nafasi ya Vijana katika Kudumisha Amani yaliyofanyika mkoani Dodoma jana. Kulia ni mtoa mada mwenzake kutoka Baraza la Dini la Kudumisha Amani, Shekh Mohammed Khamis Said.

BALOZI wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Augustine Mahiga, amesema vijana wa Tanzania ni kati ya wapiganaji wanaounda kundi la kigaidi la Al-Shabaab lililoko nchini Somalia.

Amesema kwamba, yeye binafsi amewahi kuwaona vijana hao nchini humo na kwamba aliwahi kuzungumza nao ili kujua sababu zilizowapeleka katika kundi hilo.

Balozi Mahiga ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

nchini, alitoa taarifa hiyo jana alipokuwa akizungumza na vijana mjini hapa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani.

"Nyinyi vijana ndiyo mtakaoweza kuleta amani na nyie ndiyo wenye jukumu kubwa la kulinda amani yetu.

"Kwa hiyo nawaombeni mlinde amani yetu kwa sababu kama ikitoweka itakuwa vigumu sana kuirejesha na mifano halisi ya maeneo yaliyopoteza amani mnayajua.

"Siku hizi vijana wamekuwa wakijiunga na vikundi vya kigaidi vikiwamo Al-Shabaab kwani wakati nikiwa nchini Somalia, nilishuhudia vijana wa Kitanzania wakishiriki katika kundi hilo.

"Wapo niliozungumza nao nikawauliza wamejiunga huko kwa sababu gani nao wakaniambia wanatafuta maisha. Tena Watanzania wengine niliwashuhudia wakiwa wameuawa, yaani inaumiza sana kuona wenzako wameuawa.

"Siyo kwamba vijana hao wako Al-Shabaab peke yake, wengine wako kule Yemen na tatizo hili si la Tanzania peke yake, ni tatizo la dunia kwani katika makundi ya kigaidi wako pia Wakenya na hata Waganda.

"Hili tatizo la vijana wetu kujiunga huko, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinajua kwamba kuna uandikishaji wa vijana wetu unaendelea ila hapa nilichokifanya ni kuwatonya tu," alisema Balozi Mahiga.

Katika mazungumzo yake, alizungumzia jinsi hali ilivyo mbaya nchini Somalia na kusema kuwa wakati akifanya kazi za Umoja wa Mataifa nchini humo, alisaidia kuziunganisha pande zilizokuwa zikipingana na pia alisaidia kuundwa kwa Bunge la pamoja na uwepo wa Serikali ya kidemokrasia.

"Vijana msiombe nchi ikakosa amani, wanaopigana vita hawana ubinadamu kabisa, wao hawana muda wa kula, yaani mwenzao mmoja akianguka chini, mwingine anachukua bunduki yake na kusonga mbele.

"Kwa maana hiyo, nawaomba sana muilinde amani yetu, msikubali kutumika kwa namna yoyote kwa sababu amani ikitoweka ni gharama sana kuirudisha," alisema.

Balozi Mahiga alizitolea mfano nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda, Liberia na Sieraleone ambazo alisema wananchi wa nchi hizo wanaishi maisha ya shida kwa sababu hakuna amani.

Nyerere na mapinduzi

Pamoja na hayo, alizungumzia jinsi Hayati Mwalimu Nyerere alivyonusurika kupinduliwa kijeshi katika miaka ya 80.

Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, mapinduzi hayo hayakufanikiwa baada ya vijana wawili waliokuwa wakifanya kazi mbili tofauti kutoboa siri ya mkakati huo.

"Kuna jambo sijawahi kulisema popote, lakini sasa ni zaidi ya miaka 30 ngoja leo niliseme.

"Wakati nikiwa Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, kuna kijana mmoja mwenye miaka 25 alikuwa dereva taksi alipata taarifa za watu waliokuwa wakitaka kuipindua Serikali.

"Yule kijana alipopata taarifa hizo, akamwambia mwandishi wa habari wa Daily News ambaye naye alikuwa kijana wa miaka 27. Yule kijana wa Daily News alipopata taraifa hizo, akaniambia, aliponiambia nikaanza kuchunguza ili kujua ukweli wake.

"Kwa bahati nzuri tukafanikiwa kujua ukweli na mwishowe tukawakamata hao waliotaka kupindua Serikali tukawaweka ndani ingawa baadaye walikuja kuachiwa na Rais Mwinyi.

"Kwa kweli hao vijana nitaendelea kuwashukuru na nimeamua kuwaambia hayo kwa sababu nataka mjue umuhimu wa vijana katika ulinzi wa amani nchini," alisema.

Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Gustavus Babile, aliwataka vijana kutokuwa tayari kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwa wanahatarisha maisha yao.

Alisema kwamba, kitendo cha vijana kujihusisha na biashara hiyo, kinachafua taswira ya nchi kwa kuwa ripoti za kimataifa zinaonyesha kati ya makosa 50 ya biashara za dawa za kulevya, makosa 30 yanahusisha Watanzania.

Wakati huo huo, Mwakilishi wa Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mohamed Said, aliwataka vijana wajitokeze kwa wingi wakati wa uchaguzi mkuu ujao ili wawachague viongozi bora na kuwakataa viongozi wasiofaa.
Source: Mtanzania
 
Umaskini uliosababishwa na watawala, elimu duni, kuuza viwanda vya Uma ndo chanzo cha yote
 
Yeye Amesaidia Nini ktk Kuokoa Hali Hiyo? Tuache Cheap Popularity.
 
Hizi ndizo habari za kikanjanja na tabia ya viongozi kudanganya uma.
hilo swala la dereva tax lipo kwenye kesi ya uhaini na haijawahi kuwa siri toka siku kesi ile isikilizwe

HATIBU GANDHI and OTHERS v REPUBLIC 1996 TLR 12 (CA)

Court Court of Appeal of Tanzania - Dar es Salaam
Judge Nyalali CJ, Makame JJA and Kisanga JJA

" It has been submitted to the effect that PW1 is either a liar or is in any case an unreliable witness. It was argued that it was highly improbable that the first appellant would have G divulged the coup plot to PW1, a mere taxi driver whom the first appellant had hired to drive him in the city. "

Mh. Hajatoa siri mambo yote yalikuwa wazi mahakamani
 
Huyo ni Afisa usalama Feki kwani kama angekuwa makini angeelezea hasa ni nini kinasababisha kupotea kwa amani katika mataifa mengi, angetakiwa awaase viongozi wa Africa kuacha kung'ang'ania madaraka kama wanavyofanya CCM ndani ya nchi yetu kwani kwa sasa CCM imechokwa inachofanya ni ung'ang'anizi na ndio maana wamepinga maoni ya wananchi katika huu mchakato wa katiba kwa lengo la kung'ang'ania madaraka na iwapo nchi yetu itaingia kwenye machafuko chanzo itakuwa ni CCM na si vinginevyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
I thought he explained what can abe done to prevent the flowing of Tanzanian youths to those terrorist groups na ushauri juu ya serikali za kiafrika jinsi ya kuwawezesha vijana kumbe lol.....!!
Ningekuwepo katika hayo maadhimisho ningemuuliza maswali mengi sana....
 
Niliangalia katika video za hamasa za alshabab kule YouTube naona kuna mtanzania anaitwa Mzee said anahamasisha watu wa lika zote kwenda kumpigania Allah.
 
Huyo ni Afisa usalama Feki kwani kama angekuwa makini angeelezea hasa ni nini kinasababisha kupotea kwa amani katika mataifa mengi, angetakiwa awaase viongozi wa Africa kuacha kung'ang'ania madaraka kama wanavyofanya CCM ndani ya nchi yetu kwani kwa sasa CCM imechokwa inachofanya ni ung'ang'anizi na ndio maana wamepinga maoni ya wananchi katika huu mchakato wa katiba kwa lengo la kung'ang'ania madaraka na iwapo nchi yetu itaingia kwenye machafuko chanzo itakuwa ni CCM na si vinginevyo.

Mbona unakosa busara kiasi hiki?
Unawezaje kukidharau chombo kiasi hiki?
Acheni kufuata mkumbo blindly...
 
Huyu balozi asitake kutuchanganya angesema wazi vijana wa kiislamu waliokimbia shule na kuona madrasa ndio elimu.

Hahaha umezibuka.

Balozi Dr. Mahiga kasema jumla hakutaka kuchomeka udini. Njaa haichagui dini.

Nakumbuka mwaka 1990 wakati naenda zangu shule Tambaza, pale United Nations Road opposite na kanisa la Roman Catholic St. Immaculata kulikuwa na ubalozi wa Iraq. Siku hizo ndio vita ya George Bush (the father) na Saddam inanukia.

Basi ukipita pale unaona kuna vijana kibaaaao wamekaa nje ya ubalozi eti wanataka kujiandikisha kwenda vitani.

Wengi wao walikuwa choka mbaya tu maisha ya kibongo wanataka kutafuta mchongo wa kuondokea bongo na kuitoa maisha.

Ndicho kinachoendelea mpaka leo.

I admire Dr. Mahiga's scholarship and gravitas, lakini hapa suala si tu kuwaambia vijana wasiende vitani na wailinde amani. Suala ni serikali kuweka mazingira ya kufanya vijana wawe na elimu, shughuli na ajira za kutosha kiasi kwamba isiwe rahisi kushawishika kwenda kwenye mambo ya ajabu kama vita na kuuza madawa ya kulevya.

Kijana ambaye hana elimu, kazi wala shughuli yoyote ya kueleweka ni rahisi sana kushawishiwa (hana elimu, kumshawishi si vigumu) na kuhadaiwa kwa tamaa (hana kazi/shughuli/kipato, hata ukimwambia "twende Somalia ukawe Al-Shabab, ukifuzu utapewa boat uende kuwa pirate uchukue mamilioni ya dola anakubali).

Serikali yetu yenyewe inachangia kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira yasiyo na matumaini kiasi watu waamue kwenda Somalia na Yemen huko.

Watu washapigika sana kwa bi mkubwa hapo kati kiasi kwamba ukiwaambia mtu ajichanganye hata border la Afghanistan ajichanganye na Ma Taliban anajichanganya tu.

Lowassa, with all his faults, stroke a true note when he talked about the army of unemployed youth as a ticking timebomb.
Hata wasipoenda Al-Shabab, kama vijana hawana ajira au shughuli ya maana ya kujikimu watalianzisha hapohapo bongo utasikia Kiboko Msheli imeanza, mara sijui watoto wa mbwa etc.
 
Kijana ambaye hana elimu, kazi wala shughuli yoyote ya kueleweka ni rahisi sana kushawishiwa (hana elimu, kumshawishi si vigumu) na kuhadaiwa kwa tamaa (hana kazi/shughuli/kipato, hata ukimwambia "twende Somalia ukawe Al-Shabab, ukifuzu utapewa boat uende kuwa pirate uchukue mamilioni ya dola).

Serikali yetu yenyewe inachangia kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira yasiyo na matumaini kiasi watu waamue kwenda Somalia na Yemen huko.

Watu washapigika sana kwa bi mkubwa hapo kati kiasi kwamba ukiwaambia mtu ajichanganye hata border la Afghanistan ajichanganye na Ma Taliban anajichanganya tu.

Lowassa, with all his faults, stroke a true note when he talked about the army of unemployed youth as a ticking timebomb.
Hata wasipoenda Al-Shabab, kama vijana hawana ajira au shughuli ya maana ya kujikimu watalianzisha hapohapo bongo utasikia Kiboko Msheli imeanza, mara sijui watoto wa mbwa etc.
Word .....!!
 
Hahaha umezibuka.

Balozi Dr. Mahiga kasema jumla hakutaka kuchomeka udini. Njaa haichagui dini.

Nakumbuka mwaka 1990 wakati naenda zangu shule Tambaza, pale United Nations Road opposite na kanisa la Roman Catholic St. Immaculata kulikuwa na ubalozi wa Iraq. Siku hizo ndio vita ya George Bush (the father) na Saddam inanukia.

Basi ukipita pale unaona kuna vijana kibaaaao wamekaa nje ya ubalozi eti wanataka kujiandikisha kwenda vitani.

Wengi wao walikuwa choka mbaya tu maisha ya kibongo wanataka kutafuta mchongo wa kuondokea bongo na kuitoa maisha.

Ndicho kinachoendelea mpaka leo.

I admire Dr. Mahiga's scholarship and gravitas, lakini hapa suala si tu kuwaambia vijana wasiende vitani na wailinde amani. Suala ni serikali kuweka mazingira ya kufanya vijana wawe na elimu, shughuli na ajira za kutosha kiasi kwamba isiwe rahisi kushawishika kwenda kwenye mambo ya ajabu kama vita na kuuza madawa ya kulevya.

Kijana ambaye hana elimu, kazi wala shughuli yoyote ya kueleweka ni rahisi sana kushawishiwa (hana elimu, kumshawishi si vigumu) na kuhadaiwa kwa tamaa (hana kazi/shughuli/kipato, hata ukimwambia "twende Somalia ukawe Al-Shabab, ukifuzu utapewa boat uende kuwa pirate uchukue mamilioni ya dola anakubali).

Serikali yetu yenyewe inachangia kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira yasiyo na matumaini kiasi watu waamue kwenda Somalia na Yemen huko.

Watu washapigika sana kwa bi mkubwa hapo kati kiasi kwamba ukiwaambia mtu ajichanganye hata border la Afghanistan ajichanganye na Ma Taliban anajichanganya tu.

Lowassa, with all his faults, stroke a true note when he talked about the army of unemployed youth as a ticking timebomb.
Hata wasipoenda Al-Shabab, kama vijana hawana ajira au shughuli ya maana ya kujikimu watalianzisha hapohapo bongo utasikia Kiboko Msheli imeanza, mara sijui watoto wa mbwa etc.

Ulivyonitajia Tambaza umeniongezea hasira za kuichukia Ccm, nikikumbuka msosi wa mchana ulikuwa bure nilitegemea leo watoto wetu wa Primary school wawe wanapewa maziwa ya kunywa bure kama mimi nilivyokunywa buruga ya bure nilipokuwa Nursery school.

Hivi nchi yetu tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?
 
Wakulima na wafugaji wanauana.
Je? hiyo ni amani....mbona wako kimya?
(Wengine huuliwa kimakosa wala si wafugaji wala si wakulima ni wapita njia tu)
 
Ulivyonitajia Tambaza umeniongezea hasira za kuichukia Ccm, nikikumbuka msosi wa mchana ulikuwa bure nilitegemea leo watoto wetu wa Primary school wawe wanapewa maziwa ya kunywa bure kama mimi nilivyokunywa buruga ya bure nilipokuwa Nursery school.

Hivi nchi yetu tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?

Kupenda bure kunakuja na Cost kubwa.
Maziwa ya bure umyweshwe kwa miaka! Na ccm uichukie!
Kubeli zinaharibu kichwa hassa ukichanganya na yale majani mengine.
 
Back
Top Bottom