Balozi Ngaiza Afariki dunia!


Asante sana kwa historia hiyo.

Hans Pope aliwahi kuwa Regional Police Commissioner, Iringa, na aliuawa Mutukula, karibu na mpaka wetu na Uganda, na askari wa Amin waliovuka mpaka na kutushambulia. Ilikuwa ni mwanzoni mwa 1972.
 

Nilidhani balozi wetu wa kwanza Umoja wa Mataifa alikuwa ni Akili Daniel. Nikumbushe zaidi.
 
Sikubahatika kukutana na huyu mzee ila nadhani ni baba wa Soggy Dog na pacha wake Aniceth (sijui yuko wapi huyu aliyekuwa anajiita Gaza uwanjani).

Mungu awape amani yake nasi kama jamaa zenu wa karibu tuko pamoja na nyinyi katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi!!
 

Pole sana mkulu Oscar; bahati mbaya hatujaonana tena toka tulipomaliza shule Kibaha.

Rest in Peace Balozi Ngaiza; Amen
 
Pia huyu jamaa alikuwa mshauri wa Chadema na aliwahi kugombea ubunge kupitia chadema, Mungu awarehemu wafiwa wote Amina
 
CHADEMA Kagera wamepata pigo la kuondokewa na kiongozi muhimu sana.
KAMACHUMU wamepata pigo kubwa sana kwani huyu bwana alikuwa chachu ya maendeleo katika eneo hilo. Alijenga hotel ya hadhi ya juu na kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha maji ya kunywa. Alikuwa ni chanzo kizuri cha ajira kwa watu wa eneo lake.
Mungu awatie nguvu ndugu jamaa wanae, wana CHADEMA na watanzania wote kwa msiba huu.
 

- Mkuu heshima sana na ubarikiwe!

Respect.


FMEs!
 
RIP Mzee Ngaiza............Poleni sana wafiwa




wamekwishaiondoa.............Well done Moderators/JF Admin...............

- Nafikiri ujumbe ulishafika tayari, pole sana kwa wafiwa na hasa Mkulu Oscar tupo pamoja sana katika maombolezo.

Es!
 
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mzee wetu mahali pema. Nimepata bahati ya kufanya kazi na mzee wetu mara kadhaa hususani wakati nikiwa katibu wa vikao vya kamati ya wazee. Marehemu Mzee Ngaiza alikuwa mtulivu, mwadilifu na mpatanishi-kielelezo cha uanadiplomasia wake. Lakini nitakumbuka zaidi masimulizi yake kuhusu historia hasa katika medani ya diplomasia wakati wa kipindi cha vita baridi; nilipata bahati ya kuzungumza kwa kirefu katika safari yetu ya Mkutano wa vyama vya kidemokrasia Afrika uliofanyikia Namibia yeye akiwa kiongozi wetu wa msafara. Nilitamani Mzee wetu aandike historia yake kwa kirefu kabla ya mauti kumfika. Apumzike kwa amani.

JJ
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Yesu libarikiwe.

Poleni sana Wafiwa

Mke wa Marehemu "Magdalena" Mungu akutie nguvu na akuwezeshe kupokea na kujua kuwa imempendeza Mungu iwe hivyo. Amen.
 
R.I.P. Balozi Ngaiza, wafiwa poleni sana, M/Mungu awape subira katika wakati huu wa msiba, kazi ya Mungu haina makosa.

Poleni wanaCHADEMA kwa kuondokewa na kiongozi, lakini kumbukeni msemo wa Mzee Madiba; 'unapokata mti mkubwa, basi miti mingine mingi huchipua kwenye shina lake'.
 
RIP Balozi Ngaiza.

Poleni sana Oscar pamoja na familia yote ya Balozi Ngaiza. Mwenyeezi Mungu awafariji katika kipindi hichi kigumu.


 
pole kwa wafiwa na watu wote tulio/walio guswa na msiba huu.
lakini wakati huo huo najiuliza mbona hii habari haijaandikwa kwenye gazeti lolote la tanzania?????
 
pole kwa wafiwa na watu wote tulio/walio guswa na msiba huu.
lakini wakati huo huo najiuliza mbona hii habari haijaandikwa kwenye gazeti lolote la tanzania?????

- Ndio maana some of us we believe in JF first!

Respect.


FMEs!
 
sasa mbona unatoa habari roborobo? ngaiza gani? amewahi kuwa ktk nafasi gani. kama ulimlenga oscar si unemPM ingetosha?

kama umeleta jamvini basi sema japo kidogo na wengne tujue tunamuongelea nani?

kama hujui vitu usikurupuke ku comment..kwani kama humjui si ukae kimya...ndio matatizo ya kujiunga JF hamsomi hata dos and donts mnakurupuka tu....kwani akimpa pole Oscar hapa kuna shida gani....
 
Nawapa pole wafiwa.

Nilikuwa namfahamu sana Ngaiza na alikuwa jirani pale chole road Masaki.Nakumbuka siku alipoachiwa kutoka kesi ya uhaini na furaha ya ndugu zake iliyokuwepo-(nilikuwa dogodogo wakati ule na nilimuona personally), ingawa alifungwa miaka yote hiyo, aliedelea kufanya shughuri zake kama kawaida alipoachiwa. Wengi waliousishwa kwenye kesi ya uhaini wamekwisha aga dunia, Rugakingira, kama Ngaiza, alikuwa ni mtu wa kamachumu, yeye alifariki miaka ya tisini mwishoni.

Sijui hatima ya hao wengine waliousishwa kwenye kesi hiyo, sijui ni wangapi wamebaki. Ni vizuri kama kitabu kingeandikwa kuhusu kesi hiyo na matukio hayo muhimu katika histiria ya taifa letu kabla hatujapoteza kumbukumbu!
 
.................Sijui hatima ya hao wengine waliousishwa kwenye kesi hiyo, sijui ni wangapi wamebaki. Ni vizuri kama kitabu kingeandikwa kuhusu kesi hiyo na matukio hayo muhimu katika histiria ya taifa letu kabla hatujapoteza kumbukumbu!

Ni kweli Mkuu..............hivi yule wakili Murtaza Lakha naye yuko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…