Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, tarehe 23 Februari, 2025 amefanya ziara ya kutembelea washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngazi ya jimbo katika Halmashauri ya wilaya ya Gairo. Mafunzo hayo ya siku mbili yanaendelea katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Machi 01, 2025 hadi Machi 07, 2025, katika mikoa ya Morogoro na Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.