Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
BALOZI PINDI CHANA AKABIDHI MABATI 144 SHULE YA SEKONDARI YA YAKOBI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi Mabati 144 katika Shule ya Yakobi Sekondari Mkoani Njombe.
Mhe. Pindi Chana amewaasa wanafunzi wa Shule ya Yakobi Sekondari kusoma kwa bidii, kushiriki michezo mbalimbali pamoja na kudumisha Mila na desturi za Kitanzania.
Aidha, Mhe. Pindi Chana tarehe 25 Aprili, 2023 alishiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023 katika Mkoa wa Njombe.
Mwengu wa Uhuru ukiwa mkoani Njombe utakimbizwa katika Wilaya Nne ambapo utazindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa ujumbe wa mbio hizo kwa mwaka 2023. Kauli mbiu ya mbio za Mwenge mwaka 2023 inasema “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
#Kazi Iendelee.