Zanzibar 2020 Balozi Seif: Atakayetumia Rushwa katika Mchakato wa Uchaguzi 2020, amejichimbia kisima

Zanzibar 2020 Balozi Seif: Atakayetumia Rushwa katika Mchakato wa Uchaguzi 2020, amejichimbia kisima

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
“ATAKAETUMIA RUSHWA KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI 2020 AMEJICHIMBIA KISIMA” BALOZI SEIF

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Taifa linakaribia kuingia katika Uchaguzi Mkuu ifikapo Mwezi Oktoba Mwaka huu wale waliotia nia ya kutaka kugombea nafasi mbali mbali wanapaswa kuzingatia maadili na kanuni za uchaguzi ili wapiti salama kwenye mchakati huo.

Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo wakati akizungumza na Wajumbe WA Kamati Kuu ya CCM Wilaya ya Kahama akianza ziara ya siku Tatu Mkoani Shinyanga kuangalia hitimisho la Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ndani ya Mkoa huo.

Amesisitiza suala la Umoja na Mshikamano baina ya Viongozi, Wanachama pamoja na Wananchi ili kulivua salama Taifa katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu Tanzania ikiendelea kujizolea sifa Kimataifa kwa kudumisha Demokrasia ya Vyama vingi vya Sisasa.

Mapema Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nd. Gasper Kileo ameonya kwamba wale watakaotanguliza fedha kwa ajili ya kujiweka tayari waelewe kwamba wamejichimbia kisima.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Juni 27,2020
 
Sasa kisima maana yake si una uhakika wa kupata maji ya kunywa,kuoga na shughuli zingine? Au sijaelewa

kisima kina tatizo gani?
 
Wakati Tulia Ackson akimwaga Rushwa Mbeya huyu mzee hakuona ? hivi wanadhani sisi ni wajinga kiasi hicho ! au ya Bara hayamhusu , lakini mbona kayasemea Kahama ?
 
Back
Top Bottom