ndiyomkuusana
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 666
- 426
Na Mwinyi Sadallah
16th February 2013
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, ametaka mitaala ya vyuo vikuu isaidie wahitimu vyuoni kupata ajira kwenye soko la Afrika Mashariki (EAC).
Alitoa wito huo jana akihutubia wahitimu kwenye mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Fedha kilichoko Chwaka.
Katika mazingira kama haya ni vyema vyuo vyetu vikahakikisha mitaala inakwenda sambamba na ushindani wa soko la ajira la EAC,alisema.
Aliwaambia wahitimu wa masomo ya elimu ya juu kuwa wanaongezeka lakini Zanzibar inakabiliwa na tatizo la ajira na kusababisha wasomi wengi kutegemea kuajiriwa na serikali
Balozi Seif aliwataka wahitimu wawe tayari kufanya kazi popote badala ya kukimbilia kuomba kazi Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania (TRA) kutafuta maslahi zaidi.
Aliwataka kufanyakazi kwa uadilifu na kuzingatia taaluma zao huku wakijiepusha na wizi.
Kuhusu mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika huduma za mambo ya fedha, alisema kwamba ni hatua muafaka baada ya chuo kuanzisha masomo ya Teknohama na uhasibu Zanzibar.
Akizungumzia mwamko wa jamii katika masuala ya fedha, alisema wananchi walio wengi nchini uelewa wao ni finyu hali inayokwamisha kushindwa kutumia huduma za taasisi za fedha visiwani Zanzibar.
Wazanzibar walio wengi wanafanya biashara bila ya kutumia taasisi za fedha, si kwa sababu hawapendi bali uelewa wao wa masuala ya fedha ni mdogo,alisema Balozi Seif aliyekuwa mgeni rasimi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar.
Alisema kuna baadhi ya watu visiwani hapo hawana akaunti benki na kulazimika kuhifadhi fedha kweny michago ya vitanda.
Wakati umefika kwa Chuo cha fedha kuchukua hatua za makusudi za kuelimisha umma kuhusu masuala ya fedha ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi,alisema Balozi Seif.
Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi Zanzibar, Omar Yussuf Mzee alisema serikali imeamua kukimarisha chuo hicho kwa kujenga miundo mbinu pamoja na mabweni.
CHANZO: NIPASHE