Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Naomba kuungana na Balozi wa Marekani Nchini kwa pongezi alizotoa kwa jeshi letu, kweli walifanya kazi stahiki kwa wakati.
Zipo clip zinadai askari mmoja aliyevaa kiraia nusura ashambuliwe na wenziwe, niwapongeze wananchi waliopaza sauti kuzuia polisi kushambuliana.
Lakini pia niwapongeze wananchi kwa kuweza kuzuia msafara uliokuwa unaelekea eneo la tukio, naamini tukiwekeza kukuza imani ya wananchi kwa ujasiri wao waliofanya eneo la tukio wa kuzuia vyombo vya dola baadhi ya action, lakini pia wamekuwa wepesi Sana kuweka kumbukumbu za tukio hilo kwa ujasiri mkubwa kwa ushirikiano huu tutailinda Tanzania.
Mhe. Rais hongeza juhusi kwenye community police, elekeza kufutwa kwa kesi zinazoligawa Taifa viongozi muishi kwa ushirikiano kama wanavyoishi wananchi. Ujachelewa, tumia tukio hili kuwekeza kwenye police jamii huku ukiruhusu Uhuru wa siasa na usimamizi wa haki itasaidia Sana ufichuaji wahalifu.
Otherwise niwapongeze Askari wote walioshiriki tukio like wameonyesha Dunia kwamba Tanzania tunaweza kurespond na kufanya kazi. Mhe. Rais Waite Hawa vijana wape zawadi ikiwezekana ya vyeo kutoa motisha kwa wengine, waombee nafasi za mafunzo nje waimarike zaidi na kujifunza ni hazina kwa Taifa