Balozi wa Marekani nchini Kenya atoa tamko baada ya ripoti ya Nation kufichua kuwa vyombo vya usalama vinatumia mitandao ya simu kukamata watuhumiwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Balozi wa Marekani nchini Kenya, Meg Whitman, ameonesha wasiwasi wake kuhusu ripoti iliyotoka hivi karibuni ambayo inaonesha kuwa polisi wa Kenya wanatumia taarifa za watumiaji wa simu ili kuweza kukamata wahalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Trans Nzoia, ambapo alikutana na wananchi, balozi alisisitiza kwamba nchi kama Kenya lazima iheshimu taarifa binafsi za raia.

Whitman.png

"Nimesikia kuhusu suala hili asubuhi ya leo, na ninaelewa kwamba kuna madai ya kwamba simu za watu zimekuwa zikitumika kuwatafuta na kisha kuwakamata.
Sijajua vizuri kuhusu suala hili bado. Ninachoweza kusema ni kwamba katika nchi ya demokrasia, sheria za faragha, utawala wa sheria, na haki za raia ni lazima ziheshimiwe,"
alisema Bi. Whitman.

Hivi karibuni kulikuwa na ripoti iliyotolewa na gazeti la Nation iliyofichua kwamba mashirika ya usalama wa taifa ya Kenya, kwa miaka mingi yamekuwa yakitumia data za wateja wa mitandao ya simu kwa ajili ya kufuatilia na kukamata wahalifu.

Soma pia: Kenya: Bunge laambiwa kuna Wananchi wamepata shida za Kiafya baada ya kuchukuliwa Taarifa Binafsi na Worldcoin

"Nina hakika kwamba suala hili litachunguzwa, na naamini tunapaswa kulichukulia kwa uzito kwa sababu faragha ni haki ya msingi katika nchi yoyote ya demokrasia " aliongeza.

Source: Nation Africa
 
  • Thanks
Reactions: M45

= wahalifu

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kwamba wao Marekani huwa hawaingilii mawasiliano ya watu kwa njia za simu?

Wahalifu huko wasingetumia burner phone kqma kuna uhuru kiasi hicho...
 
Wakenya wameanza kumsagia kunguni kwenye social media aondolewe na Trump
 
Back
Top Bottom