Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu amekutana na uongozi wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na Comoro - AMICAL waliofika kujitambulisha kwake. Ujumbe huo uliowajumuisha Katibu Mkuu Youssouf Said Ali ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Elimu wa Rais wa Comoro, Msemaji wa AMICAL Bwana Abdoulkader Mahmoud ambaye ni Inspekta Jenerali wa zamani wa Jeshi la Polisi Comoro na Balozi Mstaafu Mohamed Ahmed Thabit ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Waziri wa Mambo ya Nje Comoro.
Uongozi wa AMICAL umepongeza jitihada za kuimarisha uhusiano zilizopo na wameeleza utayari wao katika kusaidia kukwamua changamoto zozote zinazojitokeza hususan katika biashara na masuala ya kijamii.
Balozi Yakubu aliwaeleza namna Tanzania inavyothamini uhusiano wake na Comoro na kuahidi kukutana nao mara kwa mara na pia kuwakutanisha na viongozi wa Tanzania wanapotembelea Comoro.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwakaribisha katika Kongamano la Diaspora linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi na kushirikishsataasisi mbali mbali za Tanzania.