Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davotuglu awakabidhi Tuzo na Medani Simba Sports Club

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davotuglu amewakabidhi tuzo na medani, wachezaji ambao wamepata mafanikio katika mechi mbalimbali za timu hiyo ikiwemo tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba.

Hafla hiyo ambayo imefanyika jana usiku nyumbani kwa balozi huyo golikipa namba moja nchini Aishi Manula alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba wa klabu ya Simba.

Mbali na tuzo ya Manula wachezaji wengine walikabidhiwa medani za kuwa wachezaji bora wa mechi nne zilizopita ambao ni nahodha John Bocco ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Ndanda FC.

Mwingine ni kiungo Said Ndemla aliibuka mchezaji bora wa mechi ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar iliyopigwa mkoani Kagera na Ndemla kufunga bao moja pamoja na kusaidia jingine moja kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Hafla hiyo maalumu iliandaliwa na ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya kujenga na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Klabu ya Simba na nchi ya Uturuki.
 
Wa kimataifa orginal...
 
Sioni la ajabu hapo! Labda ulimbukeni ndo unaowasumbua
 
Yaani kupewa medani na tuzo ulimbukeni? Ama kweli Vyura mnashida
Kama ni tuzo mbona hata Makonda angewapa? Huyo balozi ni sawa na kina Slaa tu! nyie mmepagawa kunywa juice uwani kwa balozi!
 
Yanga ndio wameenda sana Uturuki. Iweje tuzo wapewe Simba, huyu balozi ni mchochezi...
 
Yanga ndio wameenda sana Uturuki. Iweje tuzo wapewe Simba, huyu balozi ni mchochezi...
Ameangalia zaidi Big Brand ya Tanzania. Kwa hivyo Simba SC ndo mahala pake
 
Kama ni tuzo mbona hata Makonda angewapa? Huyo balozi ni sawa na kina Slaa tu! nyie mmepagawa kunywa juice uwani kwa balozi!
Tuzo za Uturuki halafu atoe Makonda? Uliona wapi?
 
Tuzo ya nini sasa, huo ni ushamba kiwango cha lami.
 
Tuzo ya nini sasa, huo ni ushamba kiwango cha lami.
Bwihi [emoji16]

Yaani ni ajabu sana kuuliza kitu ambacho tayari kimeelezewa kwenye thread. Au umekimbilia kuandika tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…