Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu, amepokea ujumbe wa Meya wa Mji wa Nsujini Mstahiki Andoir Maoulana ambaye amefika ubalozini kwa lengo la kupata fursa za ushirikiano baina ya eneo lake na eneo jingine Tanzania.
Aidha Meya Maoulana aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa D’itsandra, Said Djae Karihila ambae amefika kwa minajili ya kutafuta wawekezaji katika eneo la hoteli na biashara ya vyakula na mifugo. Ubalozi umewaahidi kufanyia kazi maeneo yote hayo.