Balozi Yakubu atembelea kiwanda cha maji cha Aden nchini Comoro

Balozi Yakubu atembelea kiwanda cha maji cha Aden nchini Comoro

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Saidi Yakubu leo wametembelea kiwanda cha maji cha Aden kinachomilikiwa na Mfanyabiashara mwenye asili ya Tanzania, Khalil Bakhressa. Bw.Bakhressa aliueleza ujumbe huo kuwa hivi sasa wanazalisha maji hayo kwa wingi zaidi na wako mbioni kuanzisha kiwanda cha maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa kwa kushirikiana na kampuni za Tanzania.

Kiwanda cha Aden ni miongoni mwa viwanda vikubwa vya maji nchini Comoro.

Kwa upande wake Balozi Yakubu alimpongeza Bwana Bakhressa kwa maendeleo ya kiwanda chake ikiwa ni kielelezo cha mafanikio ya watanzania diaspora na kumuahidi ushirikiano pale inapohitajika.

IMG-20240718-WA0391(1).jpg
IMG-20240718-WA0392(1).jpg
IMG-20240718-WA0393(1).jpg
IMG-20240718-WA0390(2).jpg
IMG-20240718-WA0394(1).jpg
 
Back
Top Bottom