Balozi yakubu azungumza na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Precision

Balozi yakubu azungumza na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Precision

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Balozi wa Tanzania Nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Bw. Patrick Mwanri ambapo wamezungumzia namna bora ya kuongeza wigo wa usafiri wa anga baina ya Tanzania na Visiwa vya Comoro.

Katika mazungumzo hayo Balozi Yakubu ambaye anajiandaa kwenda kuanza kazi katika eneo hilo la uwakilishi alipokea maelezo ya safari za anga ambazo Shirika la Precision hufanya baina ya Visiwa hivyo na Tanzania mara mbili kwa wiki na pia fursa ambazo bado zipo katika sekta hiyo hasa kwa kuwa Tanzania na Comoro ni washirika wakubwa wa kibiashara.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Bw. Christian Shirima, Meneja miradi wa huduma kwa wateja.

🗓️ 08 Mei, 2024

20240509_094847.jpg
20240509_094845.jpg
20240509_094849.jpg
 
Pesa za embassy zinamfutukisha tyuu, lol
Kipipa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom