'Balozi zetu zisaidie wafanyabiashara kutafuta masoko ya nje`

'Balozi zetu zisaidie wafanyabiashara kutafuta masoko ya nje`

Mahesabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2008
Posts
6,658
Reaction score
6,700
Na Mwandishi wetu


10th June 2011


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam Wasaidizi wa Mifugo (TAVEPA), Ephrahim Massawe, ameishauri serikali kuzitumia kikamilifu ofisi zake za balozi nje ya nchi kuwatafutia masoko wafanyabishara wa Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili, Massawe amesema ofisi za balozi zina nafasi kubwa ya kuitangaza nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutafutia masoko wafanyabiashara wa nchini.
Massawe alisema wafanyabiashara wengi nchini wangependa kuuza bidhaa zao nje ya nchi, lakini kinachowakwamisha ni ukosefu wa mawasiliano kibiashara kimataifa.
“Kwa kutumia uwepo wa ofisi za balozi zetu nje ya nchi, tunaweza kutangaza biashara zetu na kupata masoko,” alisema Massawe.
”Kuna bidhaa nyingi nchini ambazo zinaweza kupata nafasi katika masoko ya kimataifa kama juhudi za kupanua sare ya masoko zitazingatiwa,” aliongeza.
Kupitia balozi hizo, Massawe alisema Tanzania inaweza kunufaika na pato la fedha za kigeni kwa kuuza mazao ya mifugo.
”Nyama ni biashara nzuri sana nje ya nchi. Lakini pia tunaweza kuuza vitu kama ngozi za wanyama, maziwa ya ng’ombe au mbuzi na vingine vingi,” alisema mwenyekiti huyo.
Akitoa mfano, alisema Somalia ambayo haina serikali ya uhakika, wafanyabiasha wake wamekuwa wakiuza mazao ya mifugo nje kwa kiwango kikubwa.
“Kwanini tusitumie balozi zetu kutafuta masoko kama Somalia iliyo kwenye mgogoro kwa muda mrefu, lakini bado wafanyabiashara wake wanafaidika na masoko ya kimataifa?” alihoji.
Massawe ambaye pia ni mwakilishi wa pekee Tanzania wa kampuni ya madawa ya mifugo ya Ufaransa inayojulikana kama Laprovet, alisema ni vyema serikali ikatazama uwezekano huo.



CHANZO: NIPASHE
 
Mabalozi wetu huko nje hata kazi zao hazieleweki wao wako busy kusubiri kuwagongea watu mihuri na kupokea mialiko ya hafla tu.
 
Back
Top Bottom