- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekutana na taarifa zinadai kuwa Baltasar Ebang Engonga ameachiwa huru na kurudi mtaani baada ya kukutwa hana hatia kwani Wanawake wale aliokuwa akifanya nao ngono kwenye zile video zaidi ya 400 ni watu wazima na walionekana kuwa wameridhia kufanya na kurekodiwa.
Aidha vipimo vilionesha hana ugonjwa wowote wa zinaa na hivyo kuwa huru kwani hajasababisha madhara yoyote kwa jamii.
Je, ni kweli au watu wanatupiga huku mtaani wakuu?
Aidha vipimo vilionesha hana ugonjwa wowote wa zinaa na hivyo kuwa huru kwani hajasababisha madhara yoyote kwa jamii.
Je, ni kweli au watu wanatupiga huku mtaani wakuu?
- Tunachokijua
- Baltasar Engonga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Fedha la Taifa (ANIF) la Guinea ya Ikweta(Equatorial Guinea), alikamatwa na kushikiliwa gereza la Black Beach akikabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za umma, kama ilivyoripotiwa na runinga ya taifa, TVGE.
Wakati wa uchunguzi wa mashtaka ya ubadhirifu wa Fedha za Umma dhidi ya mtaalamu huyu wa uchumi mwenye umri wa miaka 54, ambapo maafisa wa ANIF walifanya msako nyumbani kwake na ofisini, ndipo walipogundua video Takriban 400 za kushiriki kwake ngono na wake wa viongozi mbalimbali na wanawake walioko katika ndoa.
Video hizo zilivuja mtandaoni, na kusababisha vyombo vya habari kupaza sauti sehemu mbalimbali dhidi ya jambo hilo na Rais wa Guinea ya Ikweta, Obiang Nguema Mbasogo, alimuondoa Engonga katika wadhifa wake 6 Novemba 2024, na wote aliofanya nao ngono kufukuzwa kazi.
Baada ya kutangazwa kuwa Engonga atapimwa ili kuona kama ana magonjwa ya zinaa au lah ili kujua kama ashtakiwe kwa kuhatarisha Afya ya Umma, kumeibuka taarifa kuwa Engonga alipimwa na kukutwa hana magonjwa na hivyo kuachiwa Huru na kurudi Uraiani.
Je, ni upi Uhalisia wa madai hayo?
JamiiCheck imefatilia Taarifa hizo na kubaini kuwa hazina ukweli wowote kwani Engonga bado anakabiliwa na mashtaka yaliyomfanya akamatwe ambayo ni mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za umma, kama ilivyoripotiwa na runinga ya taifa, TVGE.
Kwa mujibu wa UGStandard Engonga alikamatwa tarehe 25 Oktoba 2024 na kuwekwa katika gereza la Malabo notorious Black Beach akituhumiwa kwa kufuja kiasi kikubwa cha pesa kutoka hazina ya serikali na kuziweka kwenye akaunti za siri katika Visiwa vya Cayman ambapo kesi yake bado inaendelea.
Kufuatia kesi hiyo, ukaguzi ulifanyika nyumbani na Ofisini kwake ndipo zilipokutwa hizo Video Takriban 400, ambapo Video hizo siyo chanzo cha kukamatwa kwake, hata hivyo hakuna chombo chochote cha kuaminika kilichoripoti kuhusu Engonga kuwa amekwisha pimwa magonjwa ya zinaa kama ilivyoagizwa ili kubaini iwapo hakuwa na magonjwa hayo.