Bana Congo ( hasa Mashabiki wa Wenge Musica zote hapa JF ) mnaniangusha mno...!!

Bana Congo ( hasa Mashabiki wa Wenge Musica zote hapa JF ) mnaniangusha mno...!!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kumbe Magwiji wote waliokuwa Wakiunda Kundi la ( Bendi ya ) Wenge Musica BCBG 4 X 4 wakiongozwa na JB Mpiana, Mpiga Solo Alain Makaba, Mpiga Bass Didier Masela, Ngiama Makanda Werrason, Adolphe Dominguez na Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wa Kizazi cha Kati Tutu Caludgi ( Yombo Lumbu ) waliamua Kuungana ( Kuurudisha Umoja wao ) na Kupiga Bonge la Concert katika Uwanja mkubwa wa Mpira huko Congo DR lililohudhuriwa na Mashabiki 75,000 ndani ya Uwanja huku Nje kukiwa na Mashabiki 45,000 waliozuiliwa Kuingia kwakuwa Uwanja ulishajaa hadi pomoni.

Imekuwaje Bana Congo Wenzangu hapa Jamiiforums ( hasa wana Wenge Musica Wenzangu ) hii Taarifa hamkuileta hapa ili tulifuatilie hilo Tamasha kwani unaambiwa kwa Historia ya Muziki Congo DR hakujawahi kufanyika Tamasha Kubwa, lililovutia Watu wengi na kuandaliwa vyema kama hili la Kukutana kwa hawa Magwiji na Mafundi wa Muziki Congo.

Inasemekana Adui yao Mkubwa Koffi Olomide aliogopa sana kusikia Tetesi kuwa Wenge Musica BCBG 4 X 4 aliyokuwa anaiogopa inarejea kwani alishajua kuwa mwisho wake Kimuziki ndiyo unakaribia kwakuwa hakuna Bendi iliyokuwa ikipendwa Congo DR na bado inapendwa kama ya Wenge Musica BCBG 4 X 4 na ndiyo maana hata ilipovunjika Koffi Olomide alifurahi sana na akaingia katika Umafia wa Kuwafarakanisha ili mradi tu wasirejee kama mwanzo.

Haya hapa GENTAMYCINE nimeanza tu ila nawaomba wale Bana Congo Wenzangu hapa Jamiiforums ( na hasa hasa Mashabiki wa Wenge Musica BCBG 4 X 4 ) mliolishuhudia hili Tamasha au Kulifuatilia mtupe Uhondo na ikiwezeka muweke kabisa na Video Clips zake na mniambie ni Duka gani hapa Dar es Salaam naweza kwenda Kununua DVD iliyokamilika ya hili Tamasha ili niwe nayo kwani nasikia lilifana sana na Misebene ya Nyimbo za Mulolo, Kine Bouge, Rhumba la Dadet, Nyimbo tamu kama za La Vie, Ave Maria, Comment Shengen, Djojo Ngonda na Filandu zilipigwa mno kiasi kwamba hakuna Mtu aliyekaa chini mpaka Kunakucha.

Pongezi nyingi ziende kwa Wanaumuziki hawa Wote waliokuwa Wakiunda Kundi zima la Wenge Musica BCBG 4 X 4 kwa Upendo mkubwa waliokuwa nao kuamua 70% ya Mapato yaliyopatikana yaende kuwasaidia Wake za Wanajeshi wa Congo DR waliokuwa Wakipambana na Waasi huko Mashariki mwa Congo DR na zingine ziende kwa Wajane na Watoto Yatima huku Wao wakichukua tu 30% ya Mapato.

Karibuni Bana Congo Wenzangu.
 
BCBG wameonyesha njia. Ni wakati sasa Wacongo Magarasa waliopo Tanzania akina Nyoshi, Bella, Patcho Mwamba, Babu Seya, Papii nk nao wapige shoo moja kuchangia mahitaji ya kibinadamu ya Wakimbizi wa Kicongo waliopo Tanzania. Waache ubinafsi na Umimi kutaka kitonga na mseleleko kwa jasho la Watanzania tuu.
All in All Wenge itabaki damuni mwangu jamaa walijua kuuupiga mwingi.
 
BCBG wameonyesha njia. Ni wakati sasa Wacongo Magarasa waliopo Tanzania akina Nyoshi, Bella, Patcho Mwamba, Babu Seya, Papii nk nao wapige shoo moja kuchangia mahitaji ya kibinadamu ya Wakimbizi wa Kicongo waliopo Tanzania. Waache ubinafsi na Umimi kutaka kitonga na mseleleko kwa jasho la Watanzania tuu.
All in All Wenge itabaki damuni mwangu jamaa walijua kuuupiga mwingi.
Umesema jambo Jema na Muhimu mno Mkuu wangu. Ubarikiwe sana.
 
Waliungana mara moja tuu kwa sababu ya show, kila mtu anaendelea na mambo yake....
Kuhusu kujaza uwanja naona kama Wacongo wanapenda muziki wao maana Fally Ipupa na Ferre Gola wote wamejaza ule uwanja...

Sent from my Pixel 4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom