Banda asubiri Tsh. Milioni 500 Afrika Kusini

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Huyu jamaa huwa kajiimarisha sana huko South Africa, na kajitahidi kudumu huko!

===

Ni wakati wa beki Mtanzania, Abdi Banda kuinjoi maisha, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na FC Richardsbay FC au Natal Rich Boys, inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini huku akiwa anasubiri mkwanja wake kutoka timu yake ya zamani Chippa United.

Banda aliingia kwenye mgogoro na Chippa United na akaishtaki Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na timu hiyo itatakiwa kumlipa Sh580 milioni ifikapo Septemba na ilikuwa ni ishu ya kimasilahi kwani alibakiza mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo.

Alizungumzia usajili huo alisema; “Ni mgeni kwenye timu siyo mgeni kwenye Ligi ya Afrika Kusini, kwani kwa mara ya kwanza nilicheza Baroka, Highlands Park nikarejea nyumbani kujipanga upya nikajiunga na Mtibwa Sugar na sasa nipo Natal Rich Boys.

“Kuhusu timu yangu ya zamani Chippa United, ni ishu ya kimasilahi na kwa sasa siwezi kuifafanua sana ilimradi nilizingatia sheria na ndio maana nikasaini mkataba na timu nyingine bila kukiuka kanuni yoyote, ninachosubiria ni kulipwa pesa yangu milioni 580.”

Alisema kipindi alichokaa nchini humo, amejifunza vitu vingi vya kuishi kama mchezaji wa kulipwa (professional), hivyo anapambana kuhakikisha anapopata fursa haifanyii mzaha, kuhakikisha anapambana kuonyesha uwezo wake.

“Mpira una muda wake, hivyo lazima nikiheshimu kipindi hiki kuona nakitumia vyema, huku wenzetu hawafuatiliwi sana nje ya uwanja, isipokuwa unasubiliwa unaonyesha wana nini uwanjani, ndio maana unakuta mchezaji anaishi kwenye misingi ya soka sana,” alisema.

Mwanachi.


Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…