Bandari D’Salaam yapoteza Sh3 trilioni kwa mwaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI

  • Fedha hizo ni sawa na asilimia saba ya pato la taifa, kitu ambacho kinawaathiri wanunuzi, wafanyabiashara na wakala mbalimbali wa Serikali


Dar es Salaam. Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikilikosesha taifa Dola 1.8 bilioni za Marekani (Sh2.8 trilioni) kwa mwaka, kutokana na kukosa ubora wa biashara.

Kutokana na hali hiyo, wataalamu wameeleza kuwa bandari hiyo inahitaji kufanyiwa maboresho muhimu ya hali ya juu, ili fedha hizo zisaidie nchi kuacha kutegemea misaada ya maendeleo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyopo kwenye kitabu cha Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania, licha ya Bandari ya Dar es Salaam kuwa sehemu nzuri, imekosa uwezo hivyo usimamiaji sera bora za kuiboresha zinatekelezwa taratibu. Ripoti hiyo inaeleza kuwa, mwaka 2012 pekee bandari hiyo ilikosesha taifa kiasi hicho cha fedha, huku ikizikosesha nchi jirani Sh1.3 trilioni.

“Fedha hizo ni sawa na asilimia saba ya pato la taifa, kitu ambacho kinawaathiri wanunuzi, wafanyabiashara na wakala mbalimbali wa Serikali,” inaeleza.

Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB), Jacques Morisset ameihimiza Tanzania kuifanya bandari hiyo kuwa moja ya vipaumbele vyake vya juu kwa ajili ya kukua kwa uchumi.

“Watumiaji Bandari ya Dar es Salaam wanalipa fedha nyingi kwa wasimamizi wa bandari na wakala mbalimbali, kwa ajili ya huduma zao kuliko Mombasa,” alisema Morisset.

Akizungumzia ripoti hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha bandari hiyo, lakini kazi ya ziada inahitajika kuifanya iweze kushindana na nyingine. “Tunahitaji nchi jirani ziendelee kuitumia bandari yetu, bado tuna kazi kubwa ya kufanya ndiyo maana niko hapa, tunahitaji kuimarisha Kitengo cha Operesheni na maeneo mengine,” alisema Dk Mwakyembe.
chanzo. Bandari D




 
"tumekuwa tukijitahidi"
kwenye kabumbu inaitwa "darizi"
endeleeni.
 
Ndo kwanza tuna mpango wa kuanza kujenga bandari MPYA Bagamoyo... wicked
 
Bwana mzizimkavu hiyo bandari yetu itazidi na itaendelea kupoteza fedha(wateja)kila kukicha,huduma mbovu ajabu mzigo wako bado utanyanyasika sana mpaka upate,leo watakwambia system ipo down kesho watatoa sababu nyingine siku zinakwenda kisha wanakudai storage,pia system yetu ya kodi ni ubabaishaji ajabu leo unatuma kitu hiki ushuru ni huu kesho unatuma kilekile ushuru tofauti kabisa,ni jana tu nimetoa container langu la futi 20,mlinzi ili uingie ndani anataka chai,mkaguzi ili alikague anataka chai,tra ndio acha kabisa,thamani ya vitu na original risiti nilikuwa nazo ilikuwa kama $4500 wao wakasema $7500 kodi iliyotoka ni 6ml nikalipia,believe me mzizimkavu nikazungushwa mpaka storage ikafika 600,000/ni wababaishaji na ni wezi pia.wakati nipo napakia container langu dubai nilikuwa na mzambia mmoja pia alikuwa na container zake 2 kwa ajiri ya shipping baada ya shipping agent kumwuliza kuwa na wewe mzigo wako unakwenda dar es salaam alicheka kidogo na akamjibu agent kuwa nanukuu 'Dar es salaam port is too much chai 'nilikuwa pale na niliona aibu sana..wateja wengi wameikimbia hiyo port hasa wale wa transit
 
Sasa zile mbwembwe za kizembe za Mwakyembe zimeenda halijojo?
 
Hakika Lucky Sabasaba umenena. TRA na policy yao ya ku- uplift charges imewafikisha pabaya, watumishi wasio waaminifu wametake advantage, huko bandarini ndo kuna uozo mkubwa sana. Waziri Mwakyembe anayo kazi kubwa sana

 
Rais wa Rwanda, mheshimiwa Paul Kagame aliwahi kusema kuwa kama akipewa bandari ya Dar es Salaam, aiendeshe kwa miaka saba, basi ataigeuza Dar es Salaam kuwa kama Dubai (kimaendeleo).
Hii yote ataifanya kwa kutumia mapato ya bandari tu.
Sasa ndio naona ukweli wa maneno yake.
 
Bwana mu israel bandari hiyo ni kweli kabisa,bandari ina thamani kubwa sana kuliko ata madini,baada ya nigeria kuwa na vijana wengi wasio na kazi,serikali yao imetumia bandari kuwakomboa,wazawa wameshushiwa kodi hivyo vijana wa kule wamebase sana katika biz ukienda dubai/china nk utakutananao wengi sana wakisafirisha mizigo,leo hii nchi za west afrika (cameroon,liberia,guine b&c,siera leon nk)vijana wao hawaendi dubai/china kununua bidhaa wanakwenda lagos...sasa sisi vijana wetu wenye bandari,tunakwenda nchi zisizo na bandari (Rwanda,Ug,malawi nk) kwenda kununua bidhaa.kuingiza kijigari kidogo kilichotumika kama vitz lazima uandae 4ml ili kuweza kukiweka barabarani !!!
 
Kwa sasa TANZANIA sio nchi ya wachache kama zamani walivyoishi babu zetu ni nchi yetu wote.
Kumuongoza mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo ni kazi kubwa.
Kwa ninavyo amini WELEDI ukizingaiwa bila kufatana fatana mambo yatasonga.
Kama maendeleo ya nchi hii ni yetu sote, kuzorota kwake kimaendeleo kunatuhusu na tusikae chini, kuuza sura, TUTAFAKARI KILA SEKUNDE TUNAVYO ITUMIA ,
"KWA RASILI MALI TULIZO NAZO HATA MOLA ATATUAADHIBU KWA KUWA MASIKINI, OMBAOMBA, TEGEMEZÎ WA WENZETU"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…