KWELI Bandari ni Suala la Muungano

KWELI Bandari ni Suala la Muungano

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hoja ya Serikali ya Tanzania kufanya Makubaliano ya awali na kampuni ya DP World ya Dubai kwenye kuendeleza bandari ya Dar Es Salaam imezua mambo mengi yanayojadiliwa sana.

Mojawapo ya Mambo hayo ni kuhusisha Bandari kuwa miongoni mwa masuala ya Muungano.

Baadhi ya watu wamekuwa wanadai kuwa Bandari ni Suala la Muungano huku wengine wakipinga.

Ukweli upoje?

IMG_7686.jpeg
 
Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

Hati ya Makubaliano ya Muungano
Msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za mwaka 1964.

Hati za Muungano zilitiwa saini na waasisi wa Muungano tarehe 22 Aprili, 1964, na kupelekea Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baada ya Muungano, Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Je, Bandari ni sehemu ya Mambo ya Muungano?
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwenye nyonyeza ya Kwanza (Mambo ya Muungano) inaitaja Bandari kama jambo la 11 kwenye sehemu ya mambo 22 ya Muungano.

Pamoja na Bandari, mambo mengine yaliyotajwa kwenye kipengele hicho ni mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

Aidha, Mwaka 2004, Serikali ya Hayati Benjamin William Mkapa ilitunga Sheria ya Bandari, inayotumika sasa (Tanzania Ports Authority Act, 2004) inayohusisha bandari zote za Tanzania, yaani Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa kunukuu, “This Act shall apply to seaports and inland waterways ports in Mainland Tanzania and Tanzania Zanzibar)

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Bandari ni sehemu ya mambo ya Muungano.

Msingi wa Mambo ya Muungano
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliainisha mambo kumi na moja ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano ambayo ni pamoja na Katiba na Serikali ya Muungano.

Mambo hayo ni Mambo ya Nchi za Nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje na Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Mambo mengine ni Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha; na Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

Uthibitisho Mwingine wa Bandari kuwa Suala la Muungano
Tunatambua kuwa Katiba ndio msingi mkuu wa hoja ya mambo ya Muungano. Hata hivyo, watu hawa pia kwa nyakati kadhaa waliwahi kunukuliwa wakithibitisha suala hili;

Oktoba 19, 2017, January Makamba akiwa Waziri wa Mazingira na Muungano alisema kuwa “Bandari ni suala la Muungano. Ufanisi wa bandari unapelekea ustawi wa Zanzibar. Ustawi wa Zanzibar unapelekea uimara wa Muungano”.

Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Mvumi (CCM) mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde na Mgombea Urais wa Mwaka 2020 kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Tundu Lissu.

Nyaraka Rasmi inayoelezea masuala 22 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza kuipata kwenye tovuti Rasmi ya Makamu wa Rais, au unaweza kuipakua hapa.

Aidha, unaweza kurejea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) kwenye sehemu ya Nyongeza.
Swali ni kuwa Jee ili hiyo hati ya Muungano iwe halali si mpaka iridhiwe na Bunge kwa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa Zanzibar

Mbona kuna ushahidi kuwa Baraza la Mapinduzi halikuidhinisha ??

Muungano wote utakuwa si Halali
 
Swali ni kuwa Jee ili hiyo hati ya Muungano iwe halali si mpaka iridhiwe na Bunge kwa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa Zanzibar

Mbona kuna ushahidi kuwa Baraza la Mapinduzi halikuidhinisha ??

Muungano wote utakuwa si Halali
Uhalali wa Muungano ni mada tofauti na mambo yaliomo na yasiokuwemo kwenye mambo ya muungano.
 
Uhalali wa Muungano ni mada tofauti na mambo yaliomo na yasiokuwemo kwenye mambo ya muungano.

Ikiwa Muungano wenyewe ni haramu , hata hizo bandari kuziingiza kwenye huo Muungano itakuwa ni haramu tu. Bandari ya Zanzibar ndio Mwinyi alimpa Mfaransa sasa kazi kwenu mnaojifanya kusoma katiba,
 
Kama mpaka leo tunamashaka juu ya Muungano wetu basi naamini watanzania ni vichwa vya wendawazimu na mlogaji ameshafariki zamani tu...
 
Sikuona kama hii ilikuwa topic kiviile. Hoja ilikuwa kwamba mkataba wa DP World unahusu na bandari za Zanzibar? Kama sio, kwa nini?
Sio wanasema wamekubalina suala la Bandari kila mmoja anasimamia bandari zake ndio maana zanzibar tayari Bandari yao wameshampa Mkaburu
 
Back
Top Bottom