unajua ushuru upo fixed tayari kulingana na kitu unachokiagiza (ambacho ni percent fulani ya bei ulionunulia, luxury products zina percent kubwa kuliko vifaa vya agriculture na computer products)na hata kama ukicheza na invoice kupunguza bei Customs wana database yao ambayo wamekadilia bei ya vitu tofauti kwahiyo wanaweza waka-uplift.
Njia cheaper ya shipment huwa ni kwa njia ya sea (meli) ambao ndio the cheapest kwa vitu vizito na vikubwa (sababu huwa wanapima kwa cubic metre) lakini ubaya wa hii njia inachukua muda mrefu sana na Bandari ya Dar uzembe mwingi ndio maana wengi huwa wanatumia bandari ya Kenya.
Kwa mizigo ambayo sio mizito sana unaweza ukasafirisha kwa kutumia air cargo (air freight) kama ni zaidi ya kg 45 lakini chini ya hapo ni vema utumie express (dhl, ups tnt, fedex etc) inakuwa cheaper na uzuri wa express wanakufanyia clearing wenyewe.
Kwa mizigo kama gari au mizigo ambayo utatumia air cargo au sea huwezi ukafanya clearing mwenyewe inabidi utumie clearing and forwarding agent (ambae atakucharge kuanzia kitu kama laki mbili kwa consignment) Sasa basi kwa huyu clearing agent wako kama ni mzuri na anajua watu bandarini mnaweza mkacheza nae na kuhonga hapa na pale na kucheza na Invoice unaweza ukajikuta labda umesave percent ya ushuru kidogo na kulipa kidogo... (lakini uwezekano mkubwa hao jamaa wa customs wanaweza waka-uplift na kusema ulinunua kwa bei ya zaidi)..
Kwahiyo ninaposema njia za panya ni zile njia ambazo hulipi ushuru au kulipa ushuru kidogo..., mfano kipindi fulani huko Sirari watu walikuwa wanapitisha mizigo usiku kwenye njia za vichochoroni na baiskeli hence hawapitii getini na hawatoi expected ushuru.