Bandari ya Bagamoyo ndio Benchmark kati ya wanaomuunga mkono na wanaompinga Hayati Magufuli

Bandari ya Bagamoyo ndio Benchmark kati ya wanaomuunga mkono na wanaompinga Hayati Magufuli

RMC

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
1,861
Reaction score
2,664
Wakati wa uhai wake Hayati Magufuli aliupinga mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na alisema nii kichaa pekee ndiye anaweza kukubali masharti ya mradi. Pia wakati wa uhai wake viongozi takribani wote wa CCM walijipambanua kama wafuasi wake kindakindaki na baadhi yao wakiwemo wabunge walipiga debe kuwa aongezewe muda apende asipende.

Sasa ghafla tu baada ya kufariki viongozi hao hao sasa wamemgeuka na wanataka bandari ya Bagamoyo ijengwe.

Kwa wana CCM ambao nwakani watafanya uchaguzi wa viongozi wao nawashauri suala la ujenzi wa bandari liwe benchmark ya kumjudge yeyote anayewaomba kura kama ni mfuasi wa JPM au anampinga. Swali liwe simple: unaunga mkono ujenzi wa bandari ya Bagamoyo au unapinga? Kila mwanaCCM apimwe kwa jibu lake moja tu kuhusu bandari. Akiunga mkono ujenzi wa bandari apigwe chini ili liwe funzo dhidi ya unafiki.

WanaCCM anzeni na kigezo hicho ili kuwafagia wanafiki.
 
Miradi iliyokamilika na ambayo inaendelea kujengwa HAINA TIJA; Mradi wa Bandari ya Bagamoyo una FAIDA kwa taifa. Loh! Hatari na nusu!!!
 
CCM doesn't exist, the late lent the green garment to thrive rescucinating the dead, but he never knew it had submicroscopic infectious agent smeared on that silently replicated the living cells. If there is anybody proud of the non-existent CCM now he/she is touting the futile to regret at the time it is too late to reverse the drifting course.
 
Aliyekuwa rais wa Urusi Joseph Stalin baada ya kifo chake alirithiwa na Nikita Khrushchev. , Siku moja Rais Nikita akiwa ana hutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi ya mtangulizi wake, Mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamuandikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "we Nikita ulikua msaidizi wa Stalin, "kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?" Nikita akakisoma na akaomba Mjumbe aliye andika anyooshe mkono juu amtambue ili amjibu .Hakuna mkono uliyo nyooshwa, Nikita akasema "kinacho kushinda wewe kunyoosha mkono leo , ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo".
C& P
 
Back
Top Bottom