Bandari Ya Dar Acheni Usiri Usio na Mpango

Bandari Ya Dar Acheni Usiri Usio na Mpango

Prof Decentman

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
276
Reaction score
140
Wadau nimesoma gazeti la daily news la leo ukurasa wa 19, taarifa kama hii niliwahi kuisoma ktk magazeti mengine. Mimi nashangazwa, nakerwa na ninasikitika kwa tabia hii ya serikali na taasisi zake kukalia taarifa,ama kutoa taarifa nusu nusu mara kwa mara. Taarifa nyingine huwa ni nzuri na hazina madhara lakini wahusika wanazificha.
Back to the point, hivi nyie bandari kila siku kutuambia habari za DRC kuwa mtumiaji mkubwa wa pili ws bandari bila kutuambia wa kwanza ni nani na watatu ni nani maana yake ni nini?
Au wa kwanza mna matatizo nae akijua mnamsifu au kumtangaza atavimba kichwa?
Mmefungua ofisi DRC na sasa nasikia mbali ya lubumbasi, kinshasa na maeneo jirani wanataka kutumia bandari ya dar jambo hilo ni zuri, ila mbona hamuweki ofisi zenu katika nchi ya kwanza na ya tatu ktk kutumia bandari.

Mnaudhi sana kutunyima taarifa sisi wananchi.
 
Back
Top Bottom