Bandari ya DSM ???

kichwat

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Posts
1,819
Reaction score
588
Wataalam wa uchumi kutoka South East Asia wanatuhakikishia kwamba Bandari ya D'Salaam PEKE YAKE inatosha kuingiza mapato ya kuendesha chumi za Burundi, Uganda, Rwanda na Tanzania yenyewe KWA PAMOJA.

Kinachotakiwa ni binadamu wenye mchanganyiko sahihi wa ELIMU, UPEO na UZALENDO (ambao hawapatikani Afrika Mashariki, hasa Tanzania).

Je, ni kweli hatuna watu wa kufanya kweli? hii ni laana au?
 
Wanaoweza kufanya hiyo kazi wapo wengi hapa Tanzania, ikiwemo hao hao walioko kazini sasa hivi. Wape new instructions na utamaduni mpya tofauti na uliopo sasa. (mambo nimesoma na kusikia kuhusu Bandari, yanafanywa makusudi, kutokana na utamaduni na uongozi), nafikiri. Na pia uchanganye na watumishi kutoka nchi zinazonufaika, watachangamka.
 
Tusubiri Mwakyembe aende pale,
Panaweza pakatufaa.
 
UPDATE: Nasikia ishu ya bandari SASA INAFANYIWA KAZI. Hongera waziri wa miundombinu!
 

Una maana gani unaposema

mapato ya kuendesha chumi za Burundi, Uganda, Rwanda na Tanzania yenyewe KWA PAMOJA
 
UPDATE: Nasikia ishu ya bandari SASA INAFANYIWA KAZI. Hongera waziri wa miundombinu!

Unatoa hongera mapema mno, kuondoa watu bila kubadili mfumo hakutabadili kitu.

Na upuuzi unaanzia juu huko kwa kina Mkapa na Kikwete.

Mkapa kauza Container Terminal, Kikwete kateua goigoi kuwa CEO.
 
Kiranga: Bandari ya DSM ikitumiwa ipasavyo (given its STRATEGIC LOCATION) inaweza kabisa kabisa kuiletea Tanzania mapato ambayo kiasi chake ni sawa na mapato ya sasa ya nchi za Burundi, Uganda, Rwanda na Tanzania kwa pamoja.
 
Kiranga: Bandari ya DSM ikitumiwa ipasavyo (given its STRATEGIC LOCATION) inaweza kabisa kabisa kuiletea Tanzania mapato ambayo kiasi chake ni sawa na mapato ya sasa ya nchi za Burundi, Uganda, Rwanda na Tanzania kwa pamoja.

This is a bold claim.

Mie naijua bandari ile vizuri sana. Unaposema "mapato ya sasa ya nchi za Burundi, Uganda,Rwanda na Tanzania kwa pamoja unamaanisha mazao yote ya goods and services yanayozalishwa na nchi hizo na kuuzwa nje as documented in their combined exports ?

Najua bandari hii ina matatizo makubwa sana, lakini ukitoa outrageous claims kama hizi kuwa specific ueleweke.

GDP ya Tanzania peke yake ilikuwa karibu USD 24 billion 2011. Hesabu za mapato ya Bandari at it's prime kwa mwaka hazikufika hata kiduchu ya hizi.

Records show


You can't even compare to a tenth of the 24 billion USD of Tanzania's GDP alone.

Msiseme vitu kijumlajumla.

Usicheze na mapato ya nchi wewe, sema kingine.
 
wenzetu kenya walishagundua udhaifu wetu. wanajenga bandari ya kisasa zaidi kwa ukanda huu huko lamu. siku sisi tukiamka kwenye mazoea.nafikiri wanaopitisha mizigo hapo dar wtakuwa wlisha hamia lamu.MUNGU ISAIDIE TANZANIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…