Bandari yetu iko bize sana au haina ufanisi

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,176
kuna meli mbili zinatarajiwa kutia nanga na kupakua mizigo bandari ya dar es salaam.

kota manisi ETA yake ilikuwa tarehe 23 septemba 2018. ni kweli iliwasili katika maji ya dar es salaam tarehe iliyopangwa. kizungu kabisa. lakini cha ajabu imekaa nje ya kidogo ya lango la kushushia siku ya tatu leo na hakuna dalili. meli hii hii ilitoka indonesia siku kadha nyuma na kufika na kuingia bandari ya mombasa bila kukalishwa foleni ikapakua na baada ya siku kama mbili ikaja huku kwetu tukaisotesa kama hivi. mpaka leo.

songa haydn nayo ina safari ya kuja kwetu. jana tu ilikuwa indonesia. leo hii ipo mombasa inapakua mzigo. haijapigwa pini. bahati ya meli hii imepangwa kupakua ticts labda itasaidia kuingia na kupakua mapema.

swali ni kwamba bandari yetu ya TPA imeelemewa na wingi wa meli kuliko bandari ya mombasa ama ufanisi ni mbovu?
 
kuonyesha msisitizo ungeweka na picha yake,ikiwa huko langoni.!!
 
Kwa ulivoona bandalini kuna meli zingine zinapakua mizigo? Tunaomba nenda kaangalie ujiridhishe kama iko busy au imepigwa pin makusud.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…