Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 180
Umesahahu kumwambia kuwa TRA wana bei zao....hiyo CIF yako toka Japan weka pembeni.....hayo mahesabu yaliyotolewa hapo juu yatakusaidia kukupa picha itakavyokuwa.......lakini jiandae na bei watakayoweka TRA ndiyo itakayopigiwa hesabu hizo hapo juu
Nashukuru mkuu na nimekuelewa fresha..Asante sana!!
Mkuu naona hapa unapotosha kidogo......TRA hawana bei yao, in principle inatakiwa waanzie kny CIF value kucalculate taxes zote kuarrive at total taxes payable, sasa kama wewe documents zako hazieleweki, ni forged etc ndio wanafanya uplifting ya CIF na sio vinginevyo.....! refer post ya Mpendanchi!
Suala la Ku-Uplift kutokana na uzoefu wangu sikuwahi kuwa na Forged Document wala nini (mara nyingi tu mimi nimeagiza gari na haya masuala yamenikuta).......suala la ku-uplift haliko wazi kabisa.......na ndio mlango mwingine wa Rushwa pale TRA.......
Mimi nazungumzia uzoefu wangu pale.......kamwe sijawahi ku-forge document........sasa kama wewe unataka mshikaji akaawaachie gari TRA wee enedelea.............
Ndg Papizo.......Jamaa wengine hapa wapo kutetea TRA pamoja na utendaji wao m-bovu...............kama walivyokuambia wengine hapo juu.........jiandae kukutana na mambo yatakayokutia HASIRA.........uwe mvumilivu......na please ni vema ukawa na pesa yako ya kutosha kama nilivyokushauri...............
Bytheway....Papizo ukisha litoa Gari lako tungependa kupata feedback mambo yaliendaje............
Nimetoa gari mara mbili, sijawahi kupata uplift au kucheleweshewa kutoa gari kiasi cha kulipia storage charge.
Kama gari ya million 4 unaandaa milioni 4 na zaidi, plus usumbufu na kusubiri muda mrefu; kwa nini usiende show room ukachague gari, ulipie vinavyopaswa the uko barabarani na mchuma wako.
Mkuu Dilunga,
Kwenye soko huria hakuna 'kwetu' wala 'ukwetu'
Nimetoa gari mara mbili, sijawahi kupata uplift au kucheleweshewa kutoa gari kiasi cha kulipia storage charge.
Kama gari ya million 4 unaandaa milioni 4 na zaidi, plus usumbufu na kusubiri muda mrefu; kwa nini usiende show room ukachague gari, ulipie vinavyopaswa the uko barabarani na mchuma wako.
nani kakudanganya?
Mkuu Dilunga,
Kwenye soko huria hakuna 'kwetu' wala 'ukwetu'
si unasikia jinsi champions wa ku-advocate soko huria jinsi wanavyobuni mikakati ya kuyabana makampuni ''yanayo ship jobs overseas''. Sasa akili kichwani, ukidanganyika kuwa soko huria ni muhimu kuliko uchumi wa nchi yako utabaki hapohapo.
Politically unaweza ukawa sahihi, lakini ktk mazingira halisi jaribu kuchukulia scenario ifuatayo; Mathalan mimi kama mwananchi mjasiriamali nimedunduliza ndururu zangu kwa miaka yote ya ujana wangu naanzisha biashara, nachukua mzigo say China nataka kuutoa bandarini, Mombasa wanataka USD 3,000 mzigo unakuwa tayari 1 week. Dar wanataka USD 6,000 + mikwaruzo na kubembeleza huduma + miezi 3 ya ucheleweshaji. Unategemea nitakubali nilipe zaidi na kucheleweshewa biashara zangu?
Huu ndio utandawazi, unatiririsha fedha kwenye route inayolipa zaidi.
Mhhh mbona kazi ipo. Sasa na kama ndiyo nataka kutoa kontena lenye personal effects (i.e. gari, nguo, furniture, electronics, etc... nimeishi ughaibuni miaka minne), ngoma yake inakuwaje? Maana nasikia kuna misamaha ya kodi kwa "returning resident" lakini hizo info sijaziona anywhere kwenye website ya TRA.