Bandarini Dar: Utoaji wa gari!



Tatizo bado lipo pale pale, tumekupa njia zinazotakiwa na mifano ya sisi tuliowahi kufanya hivyo . Ni kwamba ukifuata taratibu kama zilivyo bila ku forge chochote na kutomsikiliza the so called agent kwenye mawazo yake ya kutaka kukushauri kufanya forgery, Utafanikisha within no time.

Hata kama utakuta kumefanyiwa Uplifting ya price kama kweli ndiyo gharama halisi uliyonunulia wana kitengo pale unakwenda unatoa malalamiko yako, watakuuliza upeleke document zote original ulizoanza mawasiliano, email zote, na pay slip uliyotuma pesa!! Hapo ndipo huwa kimbembe kwa wale walio forge kwani pay slip ina gharama ingine na document zina gharama ingine. Hivyo mtu kama huyo akitoka hapo lazima atabaki kutukana na kulalamika, Lakini hatasema tatizo ni yeye.
 

... nina marafiki zangu wengi sana wanashusha gari hapo dar na kwa ujumla najuwa sana tena sana ni wasumbufu sana hapo bandarini hasa rushwa...Hicho kitu nafahamu na hata nikiileta lazima niandae hizo hela kwa ajili hiyo...

Okay, sasa kama unasema unajua yoooote hayo, na una marafiki weeeengi sana wanashusha magari, ni nini usichokijua ulichotaka kuuliza hapa ambacho hao marafiki zako wengi wanaoshusha magari hawana clue nacho?
 

Kwa ufahamu wangu, Bandari kama bandari hawacheleweshi mizigo hasa isiyokuwa containerized kama magari. Endapo umemaliza masuala ya TRA pale bandarini is a matter of hours/a day or two kupata gari lako.

Nataka nichangie ili suala la uplifting ya thamani ya gari. Kwangu mimi huu ndio mtindo unaotumika kuwaomba watu rushwa na wakati mwingine clearing agent anashirikiana na ofisa wa TRA ili wamnywe importer. Mwaka jana mwezi wa saba niliagiza gari kutoka Japan. I did not temper with documents at all. Documents kwanza zilipelekwa Tscan ambao walifanya assessment ya ushuru ninaopashwa kulipa. Baada ya kupata assessment nilikwenda benki kulipia na baada ya hapo documents zikapelekwa TRA pale long room. Baada ya siku mbili, agent wangu akanipigia simu kwamba TRA wame uplift bei ya gari kwa dola 3,000 zaidi. I could not believe it. Nilimpa agent wangu money transfer confirmation kutoka benki ili waone ni kiasi nililipia hilo gari. Hiyo document haikukubalika. Wakanitaka niwaonyeshe mawasiliano niliyoyafanya wakati naagiza hilo gari na kwa bahati mbaya sikuwa na hizo email kwani nililiagiza gari nikiwa nje ya nchi na kwa wakati huo nilikuwa sina jinsi ya kuzipata hizo email tena. Wakaniambia nilipie hilo ongezeko la ushuru halafu niidai TRA endapo nitathibitisha baadae kwamba bei ile ni ya ukweli. Wazo hilo sikukubaliana nalo. Nikaombwa nitoe chochote ili wapitishe hizo document (walikuwa wanataka Tshs. 1,750,000) nikawaambia hizo hela sina.


Baada ya siku mbili za kuvutana, nilikwenda kwa mkuu wa kitengo nikamweleza hali halisi na yeye akaagiza waangalie kwenye website ya kampuni iliyoniuzua gari ili waone kama bei ile ni sahihi. Yule afisa akaenda kuagalia kwenye internet na kurudisha majibu kwamba lile gari halipo kwenye ile website. Nikamwomba mkuu wa kitengo tuangalie pamoja kwenye internet ili niwaonyeshe lilipo hilo gari. Yule boss alikubali tukaingia kwenye ile website tusearch kwa kutumia stock number ya lile gari tukalipata. Yule ofisa akaomba radhi kwamba yeye alikuwa naangalia kwenye stock ya magari ambayo hayajauzwa. Nililazimika kulipia storage bandarini kwa siku tatu na tayari power window ziliishaibiwa.

Ninachotaka kushauri hapa ni;

1. Hakikisha unampata agent ambaye ni reputable
2. Usijiingize kwenye mchezo wa kuforge documents
3. Ukiambiwa wame uplift, dont just give up and pay
4. Hakikisha unanunua gari kutoka kwenye kampuni inayoeleweka

Wadau, nini kazi ya tscan kama wao wanafanya makadirio ya ushuru, unalipa, halafu TRA wanasema wana uplift? Kwa nini tuna Tscan then?

Tiba
 

Hiyo ya kupeleka bank slip au sijui western union tranfer confirmation TRA hawakubaliani nayo kwa sababu wengi wenye lengo la kuforge wanatuma malipo mara mbili. Mara ya kwanza anatuma kiasi ambacho anataka kionekane kwenye invoice na mara ya pili anatuma balance ambayo kwa kawaida inakuwa si kubwa kama ile ya kwanza. Hivyo hizo slip za benki TRA hawaziamini sana. Walishashtukia deal.

Tiba
 

Exactly Tiba....yaani wewe umeeleza what is TRUE on the ground...well said!!

suala linakuja.......

1. TRA/TSCAN watuambie ni kampuni gani kwao ndio reputable
2. Serikali iseme wazi umuhimu wa TSCAN kufanya assessment ambayo baadaye TRA wanakuja ku-uplift......kwa mwendo ulivyo im afraid to say TSCAN ni redundant......
 

Punda,

tatizo la uplift nimekumbana nalo zaidi ya mara tatu na nyakati zote nimelitatua kwa kufuatilia nikiwa na record zangu straight........however inanigharimu kule bandarini kwa makosa ambayo si ya kwangu.........ni wangapi wanaumia kinamna hii......i don't know......trust me kwa Tanzania yetu ilivyo watakuwa wengi tu wanaumizwa na USHENZI wa TRA

Punda......mimi nakubali tatizo la watu ku-forge docs lipo..........(binafsi sijawahi ku-forge na kamwe sitathubutu ku-forge)........lakini je solution ni ku-uplift?....what is the purpose of having TSCAN in place......

watuambie kampuni gani ambazo wao wanaziamini kuwa zinatoa bei inayokidhi threshold zao (i.e.Kile kitabu chao sijui kama unakifahamu).....kama alivyoeleza Tiba hapo juu mapaka ninatoa hizo clarity ya jinsi nilivyolipata gari langu tayari kule bandarini storage charge ina-pile up...........

Sipendi/Sitaki kukwepa kodi.......cha msingi ni kuwe na fair treatment........na UWAZI........na ninapolipa kodi hapana budi nami kujuzwa yaliyomo
 
kwakweli nami nakubaliana Tiba na ogah,

kuna njia nyingi mno zinatumika kumpa mwananchi makosa hadi afikie kutoa rushwa au pesa zaidi, mtiririko mzima haujakaa sawa, ni walewale..kuanzia agent..mwananchi hujui lipi sahihi unaishiwa kubebeshwa mzigo wa gharama! nadhani kama kila kitu kitu kikiwa wazi pakiwa na ma-agent wanaokubalika hapatakuwa na hayo matatizo ila na hilo halitawezekana kwa Tanzania yetu kila kitu kiujaujanja tu, tutaletewa theory nyingi hapa katika kujustify kuwa hakuna matatizo lakini wananchi wanazidi kulalamika...sidhani kama kuna mwananchi anayefurahia kuona gari lake linakaa bandarini miezi au kutelekeza gari bandarini!
 


Mkuu,

Sasa unaweza kutupatia majina ya hao reputable agents hapo bongo? Wengine tusije ingia mkenge.
 


Mkuuu umesema ukweli kabisa watupe kampuni maanalum ambayo wenyewe wanaijuwa ili tuweze kununua huko......Maana kwa ujumla wajamaa ni wasumbufu sana maana kila mtu anasema hivyo sasa na mimi nitaleta majibu hapa jamvini kila kitu changu kitakachoendelea!!
 
Sasa jamani hebu tusaidiane hivi tatizo kubwa zaidi je yaani ukiingiza gari lenye gharama na ndivyo wenyewe wanacharge hela nyingi zaidi au inakuwaje??Na pia nadhani mambo ya ku-uplift wenyewe wanaona ni kawaida ila kwa namna moja au nyingine nadhani inatuumiza sana sisi raia..Mfano jamaa hapo juu wamemwambia atoe 1,750,000 sasa hizo hazipo kwenye mahesabu sasa hapo itakuwaje??Kingine ni kwamba nadhani bora wenyewe watoe kampuni maalum ambayo inafahamika na wanayotaka wenyewe ili kila mtu aweze kuitumia........
 

Papizo na JF members wengine,

Katika mazingira ya kawaida, hakuna clearing agent anayepashwa kufanya hiyo biashara bila kibali cha TRA. TRA uwa wana utaratibu wa kuwaita na kuwahoji managers and wafanyakazi wa kamapuni inayotafuta kibali cha kuwa agent. Wakitosheka na competency yenu, basi wanawapa kibali cha kufanya hizo kazi. Tatizo linakuja kwamba kwa sasa clearing agent companies ziko nyingi zaidi ya wateja wanaohitaji huduma. Kila mtu aliyewahi kufanya kazi TRA akiachishwa kazi anakimbilia kufungua clearing agent company. Katika mazingira ya kukosa kazi za kufanya, inapotokea wakapata kakazi kamoja, basi wanataka waitumie hiyo nafasi kumaliza matatizo yao ya kifedha na hapo ndio mgogoro wa kujaribu kuwashauri wateja waforge documents ili kulipa ushuru kidogo linapo kuja huku wakijua mwisho wa siku TRA wataishtukia hiyo deal au agent mwenyewe anakuzunguka na kutoa siri ya mlichokifanya kwa afisa wa TRA. Kwa kujua kwamba ni kweli uliforge documents, unakubali matokeo na kukubali kutoa rushwa ili kumaliza tatizo.

Ninatoa maelezo hayo hapo juu katika kujaribu kutoa jibu la kutaja reputable clearing agents kama wadau walivyouliza. Naogopa kutaja mojawapo halafu itokee waje nao wakuingize mjini halafu mnirudie na kusema niliwa-mislead. Kuna kampuni nyingine hata ofisi hazina kabisa, ofisi ni breafcase. Ningeshauri ukitaka kumpata agent reputable hakikisha wana ofisi na wewe ufike hapo uione ofisi jinsi ilivyo then upime kama kweli watu hao wana credibility ya ku-handle mzigo wako. Kuna kampuni ambayo imewahi kunifanyia kazi vizuri bila longo longo na ofisi zao ziko pale jengo la tunakopesha opposite na parking ya magari pale city. Kwa bahati mbaya sikumbuki jina la hiyo kampuni lakini kwenye lile jengo ghorofa ya pili. Nasikia hiyo kampuni ni mali ya Bwana mmoja anayefanya kazi foreign affairs.

Tiba
 

Jamani hizi kodi zimezidi. Kwa nini ziwe juu kiasi hiki kama vile tunalinda viwanda vyetu wakati Tanzania hatutengenezi magari?

Huu ni ufisadi mwingine wa serikali yetu kuwabana walalahoi hata kwenye mitumba.

Mtumba wa 1998 bado ni WaTanzania wachache sana wanaoweza kuununua, kwa nini bado wawekewe vikwazo?

Ni lini watumishi wakawaida kama waalimu wa shule za msingi au wanafunzi wa vyuoni watakuwa na uwezo wa kununua magari kama nchi za wenzetu?
 

Hivi na wafanyakazi wa Serikali kusamehewa baadhi ya kodi wanapoingiza gari la matumizi binafsi, hii nayo imekaaje. Kwani wakulima, wavuvi ama wafanyabiashara nao hawahitaji huu msamaha wa kodi kwa gari moja?. Nadhani huu msamaha nao ungeondolewa kwa wafanyakazi wa serikali, ama basi kila mtanzania gari la kwanza binafsi asamehewe kodi.
 
NIMEWAHI AGIZA GARI ....NA NIKAELEKEZWA KWA AGENTS WALIOWAAMINIFU ZAIDI........FAITHLOGISTICS.....wapo posta ndani ya uzio wa kanisa la ANGLICAN la ST ALBANO
THE GUYS ARE TRUSTWORTH.....!
 

Mkuu,

Ni muda gani umepita toka hiyo kampuni ikufanyie hiyo kazi?
Nadhani namjua huyo bwana unaye mzungumzia, tayari amesha staafu pale, ana biashara nyingi tu lakini sikujua kama anatoa pia mizigo.
 
Wadau nilikuwa naomba kupata taarifa kwa wenye uzoefu, Je kuna formula yoyote inayotumika bandarini katika kupiga mahesabu ya ushuru wa gari kwa kutumia vigezo mbalimbali? Mimi nina mpango wa kuagiza Used Nissan X-Trail ya mwaka 2002 price yake ni dola 6000 toka Japan, 2000cc, nilipenda kupiga mahesabu ya ushuru ili nijipange zaidi.
 
tembelea gariyangu.com utaiona hiyo kanuni
 

Ntakuwekea hapa asbuhi mwanakwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…