Bank inaweza kuzuia usikopeshwe na bank nyingine?

Super H

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2012
Posts
1,070
Reaction score
405
Heshima kwenu wakuu.
Hivi ikiwa mteja anadaiwa bank "A" wanaouwezo wa kukuzuia kukopa bank. "B" ikiwa labda kule A ulitela ukorofi wa kuacha kulipa na labda wakauza dhamana etc?
na Je Bank wanaouwezo wa kublock pesa kwenye acount nyingine ya mteja bank nyingine ili kulipa deni?
_na je afisa wa bank anaouwezo wa kwenda bank nyingine kupata taarifa za mteja wa bank yao.
_Ni maswali huwa najiuliza bila majibu na natumai hapa nitapata majibu.
_senkyu!
 
Super H, Kuna kitu kinaitwa credit Bureau, huku mikopo yote kutoka bank zote huwekwa kumbukumbu. hivyo kabla ya mteja kupewa mkopo lazima wapate taarifa zako kama una mkopo bank ingine na status yake. kama uliwahi kudefault pia watapata taarifa zako. kwa hiyo yes wanaweza kukataa kukupa mkopo kwa kigezo hukulipa mkopo wa bank ingine. Kuhusu kuomba taarifa zako ama bank ingine kuzui hela zako ili zikalipie mkopo bank ingine haiwezekani na wala huwa hawabadilishani aina hiyo ya taarifa. isipokuwa kama ni taarifa za character za mteja (mkopaji sugu, msumbufu hizo wanazipata ila sio kiasi cha fedha alizonazo). huo ni uelewa wangu mdogo
 

kuna jamaa alikopa nbc akashidwa na dhamana ikauzwa tena kwa mbinde.leo amepewa mkopo nmb hii inakuweje?
 
kuna jamaa alikopa nbc akashidwa na dhamana ikauzwa tena kwa mbinde.leo amepewa mkopo nmb hii inakuweje?

Ameshalipa wa nbc tayari, kupitia hiyo dhamana yake iliyouzwa.
Angekuwa bado anadawaiwa na nbc hapo ingeleta shida.

Hata hivyo, pengine nmb hawajapata hizo taarifa za mkopo wa nbc wa huyo mteja.
 
Ameshalipa wa nbc tayari, kupitia hiyo dhamana yake iliyouzwa.
Angekuwa bado anadawaiwa na nbc hapo ingeleta shida.

Hata hivyo, pengine nmb hawajapata hizo taarifa za mkopo wa nbc wa huyo mteja.

Mkuu mwambie hivi taratibu za kumpa mteja mkopo hazijafuatwa, kuna magumashi ya 10% hapo si unajua tena mambo ya kibongobongo magumashi mengi!
loan/credit officer+manager hakucheck credit history na credit score card kuthibitisha status ya mteja.
 
Mkuu mwambie hivi taratibu za kumpa mteja mkopo hazijafuatwa, kuna magumashi ya 10% hapo si unajua tena mambo ya kibongobongo magumashi mengi!
loan/credit officer+manager hakucheck credit history na credit score card kuthibitisha status ya mteja.

mkuu. Kisima hata CRDB mnakula 10%
 
Last edited by a moderator:
Kuna aina 2 za mikopo zinazotolewa bank,moja mkopo wenye dhamana ya vitu na pili usio na dhamana ya vitu lakini kazi yako ndo inakuwa ni dhamana,katika hii aina ya pili kuna namna 2,aidha mwajiri anakata moja kwa moja kisha yeye ndo anapeleka bank au mshahara unapitia bank husika kisha wao bank ndo wanakata chao.

Ili uweze kupata mkopo yapo mambo mbalimbali yanazingatiwa mojawapo ni kupata taarifa ya kibank kutoka bank nyingine hasa kama umekuwa kwenye bank B chini ya miezi 6,na hii hufanyika kwa kumuomba mteja alete bank statement ya atleast six month toka bank A.

Na ikionekana kama amedefault sana basi mkopo ule utakuwa declined katika bank B.

Katika bank kuna system moja ya kucheki blacklist person aidha ni gaidi,jambazi,au mhalifu yoyote ambaye kimataifa amekuwa noted,lakini katika nchi yetu kuwaangalia wahalifu au wadeni sugu wa ndani ya nchi si sana labda wale ambao wanajulikana sana kitaifa,lakin hii system iko mbion kuanzishwa kwmb taarifa za mtu zitamjulishwa kiasi kwmb katika kila sekta itakuwa rahisi kupata taarifa mfano leseni ya udereva,bank,tra n.k

Kuna ujanja mwingi unafanyika kati ya loan officer na mteja,TZ kitu hakishindwi kuna watu wanajua kuzitengeza hizo bank statement acha! Wana mihuri ya kila bank,wanajua kufoji sahihi za branch managers mpka basi!!! Hivyo yawezekana jamaa yako naye alifanya hako kampango.
 
mkuu. Kisima hata CRDB mnakula 10%

Ha ha ha ha! mkuu sipo kwenye field hiyo ila nauelewa wa kutosha kuhusu mambo hayo. Kibongo bongo kucorrude hata katika sehemu nyeti ni kawaida sana!
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa ufafanuzi wenu,nimepata darasa hapa
 
je mimi ambaye mshahara wangu unapitia NMB lakini mwajiri wangu hayupo tayari kunidhamini kwenye mkopo je naweza kupata mkopo na bank ikawa inakata kupitia akaunti yangu?
 
Swali zuri sn. Ni kweli kabisa
 
je mimi ambaye mshahara wangu unapitia NMB lakini mwajiri wangu hayupo tayari kunidhamini kwenye mkopo je naweza kupata mkopo na bank ikawa inakata kupitia akaunti yangu?

Cha kwanza check na hao NMB je kampuni ambayo unafanya kazi ni miongoni mwa kampuni ambazo wameingia mkataba wa kuwapa mikopo wafanyakaz wao, kama ni ndiyo basi watakupa utaratibu wao nini cha kufanya, zaidi itatakiwa salary slip zako recently na confirmation letter toka kwa mwajiri wako kwamba wewe ni mfanyakazi wa pale.
 
Pia kuna uzi special humu wa NMB unaweza kuuutafuta ukauliza maswali humo.
 

kampuni ninayofanyia kazi haina mkataba na bank yoyote kuhusu mikopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…